Wednesday, 21 November 2012

Saturday, 10 November 2012

Sunday, 28 October 2012

Wednesday, 24 October 2012

ULINZI MKALI

 Kutokana na dunia ya leo ilivyo, kwa sasa kila kitu chahitaji ulinzi, Mali zahitaji kulindwa, afya nazo zahitaji kutunzwa. Hapa twaona swahiba kaamua kufunga ndala zake kwa kofuli ili kuzilinda. Lakini ni kweli amezipa usalama sahihi???? Hiyo yatosha watu kutoziiba au hata atakayeziiba kushindwa kuzitumia kwani????

Na ujumbe mwingine wahusisha ulinzi wa afya zetu.

Tuesday, 23 October 2012

ULISHAWAHI KUKUTANA NA HII...........


HAPPY BIRTHDAY NICKY

Tumia kifaa hiki kutambua Birthday Party inafanyikia wapi? Hakuna kiingilio

Wadau, leo ni "bethdei" yangu. Napenda kuwashukuru nyote kwa fadhila za kila namna, furaha mlizonipatia hadi nikaweza kufikia siku ya leo. Mungu awakarimu sana na tuzidi kuombeana na kushirikishana fadhila. Karibuni soda tutakiane "Maisha Marefu"

Monday, 22 October 2012

JUA KALI, HALI TATA ZA MAISHA



Kila kukicha hali ya maisha inaboreka kwa baadhi ya watu na inazidi kuwa tata kwa baadhi ya watu. Wakati wengine wanajitahidi kuboresha maisha, wengine mchana wa jua kali wanapata kinywaji asilia. Lakini tujiulize, mapumziko haya yanayosindikizwa na kinywaji hiki yanatokana na kwamba watu walishafanya kazi muda wa asubuhi, na hivyo wanastahili kupumzika au????

Sunday, 21 October 2012

JUMAPILI NJEMA

Bado mapumziko ya wiki yanaendelea, nami niwatakie jumapili njema na mapumziko mema.

Saturday, 20 October 2012

ADHA YA USAFIRI SI BONGO TU

Baada ya pilikapilika za siku nzima kuboresha maisha kwa kazi, jioni inapofika ni kipindi cha kurudi nyumbani kupumzika, lakini unapofikiria adha hii ya usafiri, uchovu unazidi. Lakini kwa wakati huo huo, kwa wenzetu hali tata ya usafiri inafanya magari kujaza sana na hata bodaboda ichukue zaidi ya abiria 7.


ASUBUHI HIVI....JIONI HIVI....


Maisha ni mzunguko. Leo mambo yapo hivi, kesho yapo vile. Japo ni mwisho wa wiki, nawasihi wadau wenzangu tuendelee kupambana kufanya maisha yaende mbele na kwa mafanikio maana mwisho wa siku nguvu zinakuwa zimepungua sana na utendaji kazi unapungu. Picha hizi zikufikirishe. Weekend njema wadau.