Tuesday, 5 July 2016

MTANGAZAJI MKONGWE MHE GODWIN GONDWE AANZA KAZI KAMA MKUU WA WILAYA

Mtangazaji mkongwe Godwin Gondwe ni miongoni mwa wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Magufuli ambaye mwishoni mwa wiki alikuwa ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya nane wa wilaya za mkoa wa Tanga walioapishwa na mkuu wa mkoa huo, Martin Shigela, kushika wadhifa huo.

Gondwe ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Handeni na hapa rasmi ameanza kutekeleza majukumu yake:

Monday, 4 July 2016

SUMBAWANGA: HAPA KAZI TU

Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

Saturday, 2 July 2016

MHE RC MAKONDA AWATANGAZIA VITA MADADA POA NA MAKAKA POA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania.

Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani

Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri

ELIMU KWANZA

Ni makosa kwa mzazi yeyote kutopeleka mtoto shule wakati serikali inatoa elimu bure kwa wote.
Yaani hata ng'ombe wanashangaa kwa nini huyu dogo hajapelekwa shule....

VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI UTATA MTUPU

MREMBO WA AFRIKA NANCY SUMARI AFUNGA NDOA RASMI

VIDEO YA MHE TUNDU LISSU:TUNAVYOTUMIA UHURU WETU

Friday, 1 July 2016

MHE RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA AWASILI NCHINI KUFUNGUA MAONYESHO YA SABASABA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Rwanda,Paul Kagame amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo na Kupokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Joseph Pombe Magufuli. Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kufanya Mazungumzo. Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja wa Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar

URENO/PORTUGAL YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA UEFA EUROPE 2016

Baada ya kutoka sare ya Ureno 1 kwa Poland 1 hata baada ya kuongezewa dakika 30, ikabidi zipigwe Penati na ndipo Ureno kupitia mchezaji wake Quaresma akafunga penati ya tano na ushindi Portugal 5 Poland 3
Pepe, Fonte na Ronaldo wakifurahia ushindi huo