Ila pia..................simu hizi zina vituko.
Huku #whatsapp kuna vituko watu na status zao:
1. Mtu ameandika “#Sleeping” , sasa leo siku ya
tano, si kashakufa huyu?
2. Mwingine kaandika “#Driving” toka mwaka jana
Agosti, naona atakuwa anakaribia China
saa hizi!
3. Haya jamaa najua kalazwa anaumwa lakini
kaandika “#Happy” we vipi ndugu yangu?
4. Huyu mdada kaandika “#Available”. Sijui anajua
maana yake? Tukikuibukia utaanza mitusi!
5. Huyu nae hajabadilisha status mwaka wa pili
sasa, “#Hey there! I’m using WhatsApp” sasa
unadhani sijui Tungekutanaje kama hutumii
Whatsapp?
6. Superstar wetu mmoja kaandika “#Urgent calls
only”. We vipi? Kwani we Fire(fanya), au
Ambulance au polisi?
7. Haka kabishoo kameandika “#Can’t talk,
WhatsApp only”. Sasa una simu ya nini? Si uitupe
uwe unashinda Facebook? Simu kazi yake ya
kwanza kuongea sio
Whatsapp!
8. Huyu mshamba kaandika “#At the movies” wiki
ya saba sasa, sinema gani ndefu hivyo wewe? Au
unafanya kazi ya kuuza tiketi hapo sinema?
9. Dogo kaandika “#At school” sasa Whatsapp ya
nini? Utapata Div O wewe!
10. Hahahahahaha eti “#Battery about to die”
miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri? Au mtaa
wenu hakuna umeme miezi sita
hujachaji simu? Si kalalamikeni TANESCO? Au
nikununulie jenereta? Unaudhi!
11. Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa nne
sasa eti “#At the gym” unajitayarisha kwa
Olympics!
12. Bosi status yako ya “#In a meeting” mwezi
mzima inachekesha, maliza huo mkutano rudi
kwenu.
WAHUSIKA BADILISHENI KABLA
SIJAWABLOCK!
Wednesday, 20 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako