Monday, 31 October 2016

ZIARA YA MHE RAIS MAGUFULI NCHINI KENYA

Rais wa Tanzania John Magufuli ameanza ziara yake ya kikazi katika nchi jirani ya Kenya leo ambapo kando na kufanya mazungumzo na Rais Kenyatta atazindua pia barabara.

Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake ikiwa ni pamoja na kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo, ambayo inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini, ni moja kati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Kenya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kuu.

Rais Magufuli akiwa nchini Kenya amewakaribisha Wakenya wote wanaotaka kufanya biashara na kuwekeza Tanzania, waje hata leo.

TASWIRA YA ZIARA

Sunday, 30 October 2016

WEMA SEPETU: MIAKA 10 BAADA YA KUWA MISS TANZANIA 2006

Hapo jana mlimbwende Wema Sepetu alihudhuria mashindani ya kumtafuta Miss Tanzania 2016 ikiwa ni miaka 10 tangu anyakue taji hilo.
Wema Sepetu 2016

Wema Sepetu 2006

MAGUFULI: UTEUZI (TANAPA NA TALIRI)

MAGUFULI: KOMESHENI MAUAJI YA WANYAMAPORI

UTAJIRI WA MGOMBEA URAIS WA MAREKANI BW. DONALD TRUMP

Trump Ocean Club International
Makazi yake
Ndege yake
Luxury Boat

MISS TANZANIA 2016

Leo kwa mara nyingine tena Tanzania imeingia kwenye Headline ya kumpata Miss Tanzania 2016 baada ya miaka miwili kupita bila kufanyika shindano la Miss Tanzania, Shindano la Miss Tanzania limefanyika Mwanza kwa mara ya kwanza na mrembo kutokea Kinondoni Dar es salaam Diana Edward Lukumai amekuwa mshindi kwa kati ya warembo 30,
(Picha kwa hisani ya Millard Ayo)
Miss Tanzania 2016 Diana Edward Lukumai
Zawadi ya gari ya Miss Tanzania 2016

Saturday, 29 October 2016

MHE RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI

HAPPY BIRTHDAY MR PRESIDENT DR JOHN MAGUFULI

Leo Oktoba 29 ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambapo alizaliwa Oktoba 29, 1959.

Rais Magufuli alizaliwa mkoani Geita na kitaaluma yeye ni mwalimu aliyebobea katika somo la Chemistry.

Katika siku yake hii ya kuzaliwa, Rais Magufuli amewashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kumuombea ambapo amesema kuwa ataendelea kufanyakazi kwa bidii na kuwatumikia watanzania wote kwa ajili ya maendelo ya nchi.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli ameandika jumbe hizi;
Follow
Dr John Magufuli ✔ @MagufuliJP
Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea.Nitafanya kazi kwa moyo&nguvu zangu zote 1/2.
10:37 AM - 29 Oct 2016
297 297 Retweets 574 574 likes
Follow
Dr John Magufuli ✔ @MagufuliJP
Ninaahidi kuendelea kufanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Mungu Ibariki Tanzania 2/2.
10:38 AM - 29 Oct 2016
218 218 Retweets 405 405 likes

Friday, 28 October 2016

SAFARI LAGER WALETA SOKONI BIA YA KOPO YA 500ml

Bila shaka umeshaliona tangazo hili matata kabisa la Safari Lager ukipita Barabara ya Kawawa jijini Dar, wajanja wanakwambia utaalamu uliotumia kutengeneza bango hilo la 3D ni wa hali ya juu sana.


Tangazo hili limekuwa likiwavutia wapita njia katika barabarani hiyo na kuwateka hisia zao, “Dah yaani hili tangazo tu lilivyo linakufanya uitafute bia yenyewe uishushe kinywani” alisikika mmoja wa muenda kwa miguu.

Sasa si tu kwamba tangazo linateka hisia na kuwa kivutio, bia yenyewe ina ladha nzuri ya aina yake na inaleta urahisi na unafuu kwa mtumiaji yeyote wa Safari Lager. Kampuni ya Bia ya TBL ilizindua bia hii ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania mwishoni mwa mwezi wa 8 mwaka huu na hadi sasa imeonekana kuwa kipenzi cha watumiaji katika maeneo mbalimbali nchini.

“Bia mpya ya kopo ya Safari ni dhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwa wakati muafaka hata wakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au kubeba akiwa anakwenda kwenye matembezi au safarini” alisema Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa

WACHAGGA BWANA........

Mchaga aliamua kufungua bustani ya wanyama akafanya kiingilio 10,000/= hakuna aliyeingia akashusha 5,000/= pia hakuna aliyeingia akashusha tena 2,000/= hakuna aliyeingia akashusha 1,000 pia hakuna aliyeingia akaamua kufanya bureeeee watu wakaingia na walikua wengi mno akafungulia Simba mmoja akafanya bei ya kutokea nje ni 20,000/=@
ALIKUSANYA HELA KAMA MCHANGA!
#WACHAGA HAWAPENDAGI UJINGA KABISA

SUMAYE: SIRUDI CCM HATA WAKININYANG'ANYA MASHAMBA

Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo halimtikisi.

Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe iliyopangiwa kesi hiyo.

“Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye anakaririwana MwanahalisiOnline.

Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.

“Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye.

Serikali imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya Sumaye shamba lake lililoko Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ameshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.

Thursday, 27 October 2016

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetangaza matokeo ya mitihani ya Darasa la saba 2016, ambapo imesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2,52. Imeitaja shule iliyoongoza Kitaifa kuwa ni Shule ya Msingi Kwema, Mkoani Shinyanga.

INGIA HAPA KUYAONA; http://necta.go.tz/matokeo/2016/psle/psle.htm


SBL YATIMIZA MIAKA 20 NA KUTOA MUONEKANO MPYA WA NEMBO YA BIA SERENGETI

Mwonekano mpya wa Bia ya serengeti katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuwanzishwa kwa Kampuni ya Serengeti Breweries Ltd mwaka 1996. Kauli mbiu ni "Taifa letu, Fahari yetu"

MHE RAIS MAGUFULI AMTHIBITISHA BW SAMWELI KAMANGA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA NIC

Wednesday, 26 October 2016

HATARI: ..............WACHINA WAMTEKA MCHINA MWENZAO DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata raia wawili wa China kwa makosa ya utekaji nyara mfanyakazi wa kasino ya Le Grande iliyopo maeneo ya Upanga, ambaye pia ni mchina aliyefahamika kwa jina la Liu Hong (48).

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro leo amewaambia waandishi wa habari kuwa, wachina hao walimteka Hong na kumfanyia vitendo vya ukatili ambapo walitoa masharti ya kupatiwa dola za kimarekani 19,000 ili wamuache huru.

Kamanda Sirro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Wang Young Jing (37) na Chen Chung Bao (35).Amesema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi katika chumba walichomficha Hong walikuta bomba la sindano, kamba za plastiki ambavyo vinasadikika kutumika kumjeruhi raia huyo wa china.

Amesema baada ya askari polisi kufanikiwa kumuokoa Hong walimpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Aidha, Kamanda Sirro ametoa taadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kuwa makini na raia wa kigeni waishio nchini kwa kuwa baadhi yao hushughulika na uhalifu ikiwemo utekaji nyara.

Amewataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna raia wa kigeni wanaonyanyasa wazawa na kufanya vitendo vya kihalifu

WEWE DADA "HATA MUNGU ANAKUONA"

Inaumiza sana kuona mtu hatumii bidii kujifunza kitu ambacho ni muhimu hasa katika maisha ya familia na anaamua kuonyesha wazi wazi kuwa yeye hayo sio fani yake. Ila kama mwanamke wa kiafrika na unaejua nafasi yako katika familia, "Jitume".

MOROCCO NA TANZANIA KUSAINI MIKATABA 21 YA USHIRIKIANO KTK ZIARA YA MFALME WA MORROCO

Mfalme Mohammed VI wa Morocco amekubali maombi ya Rais John Magufuli ya kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma ambao utakuwa mkubwa kuliko ule wa Taifa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga msikiti mkubwa jijini humo.

Rais Magufuli aliyasema hayo Ikulu Dar es Salaam jana wakati akitoa shukrani baada ya kukutana na kiongozi huyo, aliyeambatana na wajumbe 150 ambao pamoja na mambo mengine, nchi hizo mbili zilisaini Mikataba ya Makubaliano (MoU) 21.

Akitoa taarifa fupi ya mazungumzo baina yao, Rais Magufuli alisema Mfalme Mohammed VI amekubali kujenga msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 80 (zaidi ya Sh bilioni 160).

“Katika mazungumzo yetu, nimshukuru Mfalme Mohammed wa Morocco amekubali ombi langu la kujenga msikiti mkubwa hapa Dar es Salaam, na amekubali kwenye mji mkuu Dodoma, atajenga uwanja wa mpira utakaokuwa mkubwa kuliko wa Dar, na thamani yake ni zaidi ya Dola milioni 80,” alieleza Dk Magufuli.

Uwanja wa Taifa umejengwa na Wachina kwa gharama ya Sh bilioni 60 na una uwezo wa kuchukua watu 60,000 waliokaa. Dodoma ambayo ni Makao Makuu ya nchi na Serikali ya Awamu ya Tano imepanga yote kuhamia huko ifikapo mwaka 2020, inao Uwanja wa Jamhuri ambao unamilikiwa na CCM na unachukua watu 8,000.

Mbali na hayo, katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili kwenye nyanja ya usalama na ulinzi, Mfalme huyo amekubali kuanzisha programu ya kubadilishana mafunzo baina ya askari wa Tanzania na Morocco na kwa kuanza wiki ijayo askari 150 wa Tanzania watakwenda mafunzoni nchini Morocco.

Katika ziara ya siku tatu ya kikazi ya Mfalme Mohammed VI aliyewasili nchini juzi, akiwa na ujumbe wa wafanyabiashara pamoja na viongozi wengine, wamefanikiwa kufanya makubaliano ya mikataba 21 katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kilimo, gesi, madini na na usafiri wa anga.

Mikataba hiyo ni pamoja na Makubaliano ya Jumla katika Ushirikiano wa Uchumi, Sayansi, Ufundi na Utamaduni baina ya Serikali ya Morocco na Tanzania yaliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga na Waziri wa wizara hiyo wa Morocco, Salahddine Mezouar.

Mwingine ni ule wa kuanzishwa kwa Jukwaa la Mashauriano ya kisiasa baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wizara hiyo nchini Morocco, mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya gesi, nishati, madini na sayansi ya miamba, mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa anga, mkataba wa ushirikiano kwenye mradi wa mtangamano wa kuwasaidia wakulima wadogo nchini.

Pia mkataba wa makubaliano kwenye sekta ya uvuvi, mkataba wa makubaliano baina na MASEN-Morocco na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya maendeleo ya nishati mbadala, mkataba wa ushirikiano baina ya Shirika la Mbolea la Morocco (OCP) na Shirika la Mbolea la Tanzania katika kuendeleza soko la mbolea na kilimo nchini.

Pia mkataba baina ya Bodi ya Utalii Tanzania na Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Ofisi ya Utalii ya Taifa nchini Morocco, Mkataba wa Kundi la Utoaji Mikopo la Morocco na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Mkataba baina ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Shirika la Bima la Morocco.

Mingine ni Mkataba wa Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (EPZA) na Kundi la SNTL la Morocco katika ubia wa uendelezaji na utangazaji wa viwanda, mkataba wa usafirishiaji kwenye reli kupitia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RACO) kwa ajili ya ubia kuendeleza reli ya Mtwara-Mchuchuma/Liganga.

Aidha, mkataba mwingine ni ule wa kuanzishwa kwa Baraza la Biashara baina ya Shirikisho la Wafanyabiashara wa Morocco (CGEM) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mkataba wa Mkopo baina ya Benki ya Afrika (BOA) na Hospitali ya CCBRT na mkataba wa mkopo wa BOA na Kampuni ya gesi ya Lake.

Mkataba wa Mkopo wa BOA na Kampuni ya Superstar Forwarders, Mkataba wa Ushirikiano baina ya Kampuni ya OLAM Tanzania na Benki ya Attijariwafa, mkataba wa ubia baina ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)na Benki ya Centrale Populaire ya Morocco, mkataba wa Kitaalamu baina ya Shirikisho la Bima la Morocco na kampuni za bima Tanzania.

Pia mkataba wa ushirikiano baina ya kampuni ya kuchanganya chai ya Morocco na Kampuni ya Afri Tea and Coffee ya Tanzania.

Akizungumzia MoU kwenye usafiri wa anga, Rais Magufuli alisema wamekubaliana nchi hizo mbili kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwenda Rabat, mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

“Na sisi tumeanzisha shirika letu kidodokidogo linasuasua, lakini tutakuwa na ushirikiano mzuri na Shirika la Ndege la Morocco, na makubaliano haya yote ni mwelekeo nzuri wa kuijenga Tanzania na kuwa na uchumi unaokua kwa asilimia 7.2,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema Morocco imepiga hatua kubwa kwenye utalii na kwamba mwaka 2015 ilipokea watalii milioni 10.5 na mwakani wanategemea kupokea watalii zaidi ya milioni 14 na kwamba Tanzania imesaini makubaliano kwenye sekta hiyo kwa lengo la kuendeleza hifadhi za nchi na kuutangaza utalii.

Aidha, alisema makubaliano yote hayo yamelenga kuijenga Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda na kwamba hilo linawezekana kwa kuwa hata sasa hali ya uchumi wa nchi ni nzuri kwa kuwa unakua kwa asilimia 7.2; na taarifa za uchumi zinaonesha kwenye robo ya pili ya mwaka uchumi umekua kwa asilimia 7.9.

“Tuko kwa ajili ya kuujenga uchumi na niwakaribisheni wageni wetu kutoka Morocco, niwahakikishieni kuwa mko salama na karibuni kuwekeza kwa faida ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wake ulianza tangu enzi za Iban Batutu wa Morocco aliyetembelea Kilwa miaka mingi iliyopita,” alieleza Rais Magufuli.

BODABODA HAWAISHIWI MANENO

Monday, 24 October 2016

MHE BEN SITTA (CCM) NDIO MSTAHIKI MEYA MPYA WA KINONDONI

Meya mpya wa Kiondoni Mstahiki Ben Sitta, baada ya kushinda uchaguzi huko kwa kishindo jana

MTUKUFU MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU 7

chini ni sehemu ya ujumbe wa wafanyabiasha wa Morroco

Sunday, 23 October 2016

UDAKU: HII INATOKEA TU TANZANIA

Ni Tanzania tu ambapo mdada anajua kabisa tarehe ya kuvalishwa pete ya uchumba (engagement), anashona nguo, na anakwenda saluni, halafu mwanaume mchumbiaji anapokuja na shamrashamra zote siku ya tukio, eti akitoa pete kumvalisha mdada huyo anajifanya kushangaa sana (SURPRISED)! Kuna mmoja alizimia kabisaa wakati ni yeye ndiye aliyetafuta mpaka sonara! TUNAISHI KWA KUIGIZA!..😂😂😂😂

Saturday, 22 October 2016

MRADI MKUBWA WA HOTELI YA KITALII KUJENGWA HUKO MATEMWE ZANZIBAR

Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar.

MHE RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI HOSTEL ZA UDSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Oktoba, 2016 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho.

Wakati Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.

STAA WEMA SEPETU KUNA KITU ANATAKA KUSEMA HAPA

Inawezekana ndoa inanukia

Thursday, 20 October 2016

Monday, 17 October 2016

BAADHI YA WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAM NCHINI NIGERIA WAREJEA

Aprili 2014 zaidi ya wasichana 270 walitekwa wakiwa shuleni katika mji wa Chibok na wapiganaji wa Boko Haram, mpaka leo ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana hao, Alhamisi ya October 13, 2016 ziliripotiwa taarifa za kuachiwa kwa baadhi ya wasichana hao na kurejeshwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa serikali ya Nigeria na viongozi wa Boko Haram.

Leo October 17 2016 Wasichana 21 wa Chibok hatimaye wamekutana na familia zao