Sunday, 28 October 2012

Wednesday, 24 October 2012

ULINZI MKALI

 Kutokana na dunia ya leo ilivyo, kwa sasa kila kitu chahitaji ulinzi, Mali zahitaji kulindwa, afya nazo zahitaji kutunzwa. Hapa twaona swahiba kaamua kufunga ndala zake kwa kofuli ili kuzilinda. Lakini ni kweli amezipa usalama sahihi???? Hiyo yatosha watu kutoziiba au hata atakayeziiba kushindwa kuzitumia kwani????

Na ujumbe mwingine wahusisha ulinzi wa afya zetu.

Tuesday, 23 October 2012

ULISHAWAHI KUKUTANA NA HII...........


HAPPY BIRTHDAY NICKY

Tumia kifaa hiki kutambua Birthday Party inafanyikia wapi? Hakuna kiingilio

Wadau, leo ni "bethdei" yangu. Napenda kuwashukuru nyote kwa fadhila za kila namna, furaha mlizonipatia hadi nikaweza kufikia siku ya leo. Mungu awakarimu sana na tuzidi kuombeana na kushirikishana fadhila. Karibuni soda tutakiane "Maisha Marefu"

Monday, 22 October 2012

JUA KALI, HALI TATA ZA MAISHA



Kila kukicha hali ya maisha inaboreka kwa baadhi ya watu na inazidi kuwa tata kwa baadhi ya watu. Wakati wengine wanajitahidi kuboresha maisha, wengine mchana wa jua kali wanapata kinywaji asilia. Lakini tujiulize, mapumziko haya yanayosindikizwa na kinywaji hiki yanatokana na kwamba watu walishafanya kazi muda wa asubuhi, na hivyo wanastahili kupumzika au????

Sunday, 21 October 2012

JUMAPILI NJEMA

Bado mapumziko ya wiki yanaendelea, nami niwatakie jumapili njema na mapumziko mema.

Saturday, 20 October 2012

ADHA YA USAFIRI SI BONGO TU

Baada ya pilikapilika za siku nzima kuboresha maisha kwa kazi, jioni inapofika ni kipindi cha kurudi nyumbani kupumzika, lakini unapofikiria adha hii ya usafiri, uchovu unazidi. Lakini kwa wakati huo huo, kwa wenzetu hali tata ya usafiri inafanya magari kujaza sana na hata bodaboda ichukue zaidi ya abiria 7.


ASUBUHI HIVI....JIONI HIVI....


Maisha ni mzunguko. Leo mambo yapo hivi, kesho yapo vile. Japo ni mwisho wa wiki, nawasihi wadau wenzangu tuendelee kupambana kufanya maisha yaende mbele na kwa mafanikio maana mwisho wa siku nguvu zinakuwa zimepungua sana na utendaji kazi unapungu. Picha hizi zikufikirishe. Weekend njema wadau.

Friday, 19 October 2012

KARIAKOO HALI SI SHWARI





Habari za hivi punde zinadai kuwa kuna hali mbaya katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar e Salaam ambapo polisi wanapiga mabomu ya machozi kutawanya waislam wanaoandamana.
Kwa mujibu wa watu waliopo kwenye maeneo hayo maduka mengi yanafungwa na watu wanajifungia kwenye maduka hayo. Ingia hapa kwa taarifa zaidi:http://www.bongo5.com/breaking-kariakoo-pachafuka-mabomu-yanapigwa-kila-kona-10-2012/

KARIBUNI MLO WA MCHANA (LUNCH)

Wadau leo inabidi twende mpaka Bukoba ili lunch yetu inoge

NILIJUA UTACHEKA!


Jamaa watatu walikodi hoteli yenye gorofa 60, wao wakapata gorofa ya mwisho kabisa. Wakapanda kwa lifti na asubuhi wakashuka kwa lifti. Jioni waliporudi wakakuta umeme umekatika.
Wakakubaliana wapande ngazi kwa story. Wa kwanza akapiga story za kutisha kuanzia gorofa ya 1 mpaka ya 20, wapili akapiga strory za kuchekesha kuanzia gorofa ya 21-40 na watatu akandamiza story za kuhuzunisha kuanzia gorofa ya 41-60. Walipofika ya 59 yule watatu akasema hii ndio ya kuhuzunisha zaidi...TUMESAHAU KUCHUKUA FUNGUO PALE MAPOKEZI.

Hapa jamaa kaona kawin kweli kweli, kumbe hasara za kukumbia umande......soma kaka soma

ASUBUHI NJEMA

Labda tuanze siku yetu na kutafakari picha hii inayosisitiza kufungua macho. Watani wanasema, "kusoma hujui, hata picha nayo huioni"???

TUIGE LAKINI..........

Kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ipo katika mchakato wa kupigia kura baadhi ya vivutio vilivyopo nchini(Serengeti, Ngorongoro, Mlima kilimanjaro, fukwe za zanzibar, mapango ya Amboni n.k.), ila walau kimojawapo kiingizwe katika orodha ya maajabu ya Dunia. Tuangalie na hiki kisijekuwa mojawapo ya maajabu.

Tuesday, 16 October 2012

SHULE JAMANI SHULE

Hata baada ya miaka 50 ya Uhuru, nchi yetu inajitahidi kutengeneza maisha bora kwa kila mtanzania,. Hii ni pamoja na kuboresha elimu na mazingira yake, lakini kwa mtindo huu itwakuwaje???

HII NAYO KALI

Jeshi la Polisi nchini China
Polisi wa kike Marekani


Polisi nchi fulani Afrika

YA KWELI HAYO???

Ni kweli wa Moshi twapenda kutafuta hela, lakini tafsiri hii kiboko.

HABARI ZA ASUBUHI KUTOKA BAGAMOYO


Wapendwa wadau, ni asubuhi sasa, nami kutoka Bagamoyo, nawatakia asubuhi njema na kazi njema.

Monday, 15 October 2012

YALE YALE Tutatokaje katika hali hii duni katika kila sekta ya maisha.....
KARIBUNI BAGAMOYO Katika matembezi yangu Mji wa kale Bagamoyo, nilifanikiwa kutembelea sehemu iitwayo $Kaole Mamba Ranch$ na kukutana na hawa.
HODI TENA Kutokana na pilika pilika za maisha, kwa kipindi fulani imekuw avigumu kuwa mtandaoni. Kwa sasa nimerejea tena katika ulingo kuwaletea za leo leo kutoka nyumbani na popote duniani. Karibuni wadau