Friday, 31 July 2015

BARABARA KIA - MERERANI KUJEGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

Baada ya kilio cha muda mrefu kuomba wajengewe barabara ya Kia-Mererani kwa kiwango cha Lami, Serikali kupitia Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli amekamilisha maandalizi na hivyo ujenzi kuzinduliwa rasmi leo. Barabara hii ni muhimu itokayo Kiwanja cha Kimataifa cha ndege cha Kilimanjaro,kwenda yapatikanapo madini ya TANZANITE.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi

KUJIREMBA MUHIMU, ILA HII KALI

AMECHUKUA TENA. NANI?.....NINI?.....

Mhe Edward Lowassa aliyekatwa CCM na kuamua kuhamia CHADEMA, leo amechukua Fomu ya kuomba kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho.
Mhe Lowassa akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA mhe.Freeman Mbowe mara baada ya kukabidhiwa Fomu za urais

Thursday, 30 July 2015

KAULI YA ZEMBWELA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015


SINA CHAMA SINA KADI ila..
Taifa lina KIU.....MIMI nadhani tunakosa na linahitaji mtu mwenye SIFA 3

1: Asiye na MAKUNDI ili asilipe FADHILA kwenye UTEUZI wake.

2: Atakae weza kutupeleka MWENDO MDUNDO kuanzia MFANYAKAZI wa ndani mpk MFANYAKAZI wa BOT, TRA, nk

3; Taifa linahitaji Rais mwenye UWEZO wa KULITAFUNA ''JONGOO''

KUTOKA MAGAZETINI

ASEMAVYO DR.SLAA KUHUSU MHE.LOWASSA

Tuelewe kipi sasa?. Mmemponda Lowassa, kisha mmempokea CHADEMA

RAIA WA KICHINA WAKAMATWA DAR WAKIUZA MAJI MACHAFU

Raia wawili wa Kichini, mke na mume wamekamatwa Jijini Dar wakiwa wanajaza maji kwenye chupa zilizotumika tayari kuyauza tena.

Tuesday, 28 July 2015

UKAWA KUMEKUCHA, LOWASSA NAE YUMO


LOWASA - "Kuanzia leo naondoka CCM, nitikia wito wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.. niungane nao katika kuleta mabadiliko. Namshukuru sana James Mbatia.
Sikufanya uamuzi huu kwa pupa. Nimejiridhisha ndani ya UKAWA ndio kuna fursa pekee kushinda uchaguzi.. tutaondoa uhodhi wa chama kimoja.
(akimnukuu Nyerere) ...CCM sio Baba wala Mama Yangu.. wanaCCM kama wanataka mabadiliko wayatafute nje ya CCM, na mimi CCM sio Baba wala Mama yangu"
Mhe Edward Lowassa akiongea na waandishi wa habari na mamia ya watu wengine waliofurika katika Hotel ya Bahari Beach, alipokuwa anatangaza nia yake ya kujiunga na CHADEMA

MHE. LOWASSA KULIKONI???


Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema umemkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kujiunga nao katika harakati za kuking'oa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Saturday, 25 July 2015

WEMA SEPETU ASHINDWA KURA ZA MAONI UBUNGE VITI MAALUM CCM SINGIDA

Msanii wa Filamu za kibongo anayeongoza kwa urembo ndani ya tasnia hiyo, Wema Abraham Sepetu, aliyekuwa anagombea Ubunge wa Viti Maalum jimbo la Singida amebwagwa chini baada ya kupata kura 90 tu katika uchaguzi huo.

Mgawanyo wa kura ulikuwa hivi;
1. Aysharose Mattembe (311)
2. Martha Mlata(235)
3. Diana Chilolo(182)
4. Wema Sepetu(90)

MHE. RAIS OBAMA ZIARANI KENYA


Mhe. Rais Barack Obama wa Marekani akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwa ajili ya kufungua mkutano wa Kimataifa wa kibiashara, Ugaidi na haki za binadamu unaofanyika nchini humo kabla ya kuendelea na ziara yake nchini Ethiopia
Hapa Mhe. Rais Barack Obama akisalimiana na mwenyeji wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na bibi yake Mama Sarah Obama kushoto na dada yake Auma Obama katika chakula cha jioni na wanandugu wa familia ya Obama nchini Kenya Baba mzazi wa Barack Obama ni mzaliwa wa Kenya

ASEMAVYO MHE.J.P.MAKUFULI

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amesema akifanikiwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa juu wa nchi hii, atahakikisha anatekeleza ipasavyo Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho.
Alisema hayo mjini hapa jana jioni alipokuwa akisalimiana na mamia ya wananchi, walioenda kumwona akiwa safarini kutoka nyumbani kwake Chato mkoani Geita kuelekea Dodoma. Alisema ni kwa kutekeleza kikamilifu Ilani hiyo, ndipo maendeleo ya kweli nchini yatapatikana.
Hata hivyo, alisema kuwa atahakikisha analeta maendeleo kwa watu wote bila ubaguzi wa dini, rangi, kabila wala itikadi.
“Maendeleo hayana Chama. Nikifanikiwa kuwa Rais nitaleta maendeleo kwa kila mtu... Kwa wana-Chadema, Wana-Cuf na hata kwa wale wasio na Chama,” alisema Dk Magufuli.
Aidha, alisema akifanikiwa kuwa Rais, atakuwa mtumishi wa watu na kuhakikisha anachagua serikali ya watu makini wasioonea wananchi.
“Namwomba Mwenyezi Mungu nisije kuwa Rais wa kujikweza, wa kujivuna na wa kusahau watu wangu” alisema Dk magufuli.
Dk Magufuli aliwakosha wananchi na kushangiliwa kwa nguvu pale alipotiririka kwa salamu za makabila mbali mbali nchini, kuanzia Kaskazini hadi Kusini, Mashariki hadi Magharibi mwa Tanzania “Huo ndio Utanzania wetu,” aliwaambia wananchi baada ya kumaliza na kuongeza kuwa atahakikisha anazingatia na kudumisha misingi yote mizuri, iliyoachwa na waasisi wa Taifa hili na marais waliopita.

MHE. ESTA BULAYA (CHADEMA) AANZA KUWASHA MOTO BUNDA

Mhe.Esta Bulaya aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum CCM akiwahutubia wananchi wa Bunda ambapo ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya CHADEMA

Friday, 24 July 2015

KAZI NA DAWA

Inaonekana ndizi hiyo haibebeki bila KIROBA (Konyagi)

Wednesday, 22 July 2015

WABUNGE WAWILI CCM WATIMKIA CHADEMA RASMI

MBUNGE WA KAHAMA mzee James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalum Easter Bulaya
Mhe James Lembeli akiwapungia mikono wananchi alipokuwa anawasili kwenye mkutano huko Mwanza
Pembeni ni Mbunge wa Ubongo mhe. John Mnyika

MHE RAIS KIKWETE AKABIDHIWA JOHO NA CHETI CHA SHAHADA YA "DOCTOR OF LAWS"

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akimkabidhi Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rais joho na cheti iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maprofesa waandamizi wa chuo hicho.Tayari Rais Kikwete alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Octoba mwaka 2011
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandakla pamoja na maprofesa waandamizi wa chuo hicho muda mfupi baada hafla fupi ya kumkabidhi Rais Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha kwa hisani ya Freddy Maro)

Tuesday, 21 July 2015

Sunday, 19 July 2015

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Tunapoendelea kusherehekea Eid, ikiwa ni siku ya Jumapili pia tujipe moyo kwa kutokata tamaa katika yale tufanyayo kila siku ili mradi ni mema. Mungu yupo pamoja nasi. Tazama wengine ambavyo wanajitahidi. Tumia neema ulizojaliwa na mungu kwa manufaa-maendeleo yako na jamii kwa ujumla.

DK. MAGUFULI APOKELEWA KWA SHANGWE MWANZA

Mke wa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM, Janet Magufuli akiwasalimu wananchi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kuja kumuona mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli.

Saturday, 18 July 2015

SIKUKUU YA EID INDIA HAPATOSHI

Watu wenye asili ya kihindi wakigombania usafiri wa treni nchini humo wakiwahi makwao kusheherekea siku ya Eid na familia zao

"EID MUBARAK". NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA

ADHA WAPATAYO KINAMAMA HASA WA VIJIJINI

Ni matumaini yetu kuwa Serikali itakayoingia madarakani hapo Oktoba itajitahidi kusaidia kupunguza adha hii ya maji. Poleni sana kinamama wote mnaoteseka kwa tatizo jili la kufuata maji umbali mrefu.

Friday, 17 July 2015

SAFU YA URAIS CCM YAENDA KUTAMBULISHWA ZANZIBAR

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.
Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.