Mama alijitahidi kula vyakula bora,kulala kwenye chandarua, kula mbogamboga za majani, na matunda, alijizuia kufanya kazingumu ili wewe uzaliwe salama. Ukakaa tumboni kwake miezi tisa, siku yake ilipofika, hakubana miguu, hakukataa kwenda hospitali, alilia kwa uchungu, alinyofoa hadi nywele za kichwa chake kwa uchungu, ili wewe mtoto uzaliwe, alibana pumzi ya uhai wake ili wewe uzaliwe.
Haikutosha, alikulea kwa taabu na shida, alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yako, alikulea
kwa upendo, ukasoma, mme wake ambaye ni baba yako alikukataa ukiwa mdogo, kwa shida na kujibana huku akifanya kazi usiku kucha akakukuza na ukakua, ukafikia umri wa kutambua baya na jema.
Leo hii eti unapigana na mama? unamdharau mama?Una maisha mazuri, una kazi nzuri, lakini unashindwa kumhudumia mama? Unaishi katika nyumba nzuri, ya kifahari, mama yako analala kwenye nyumba inayovuja? Jua na mvua vyote vyake? jaribu kuiheshimu na kuithamini thamani ya mama katika dunia hii..
Hakuna kama mama na hatatokea, mpende sana mama yako sasa!! Na kama huna maelewano mazuri na mama yako, ni muda wa kujirekebisha na kujirudi kwake ukiomba msamaha na kuumia kwa kitendo hicho . Nani kama mama?
Sunday, 10 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako