Monday, 25 May 2015

CCM YATANGAZA MASHARTI KWA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI KWA UCHAGUZI UJAO

*Mbwembwe,sherehe marufuku
*Idadi ya wadhamini, mikoa sasa yaongezwa
*Wajumbe NEC, marufuku kudhamini wagombea
Chama cha Mapinduzi(CCM), kimetangaza rasmi ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya urais, huku kikitoa masharti magumu kwa wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho.
Chama hicho kimetoa msimamo wake kuwa wagombea wanatakia kuheshimu kanuni na misingi ya chama hicho na ni marufuku kwa wagombea kufanya mbwembwe, madoido na kukodi watu kwa ajili ya kukushangilia wakati wa kuchukua fomu au kurudisha ni marufuku.
Akitangaza uamuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu(NEC) ya chama hicho, leo mjini Dodoma,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema fomu ya kugombea urais itaanza kutolewa Juni 3 mwaka huu na kuzirudisha Julai 2 mwaka huu saa 10 jioni.
Amesema kuanzia Juni 3 wanaruhusiwa kuanza kuchukua fomu na kuzirudisha Julai 2 mwaka huu. Wakishachukua fomu watafanya kazi ya kutafuta wadhamini mikoani.
Amesema mwaka huu idadi ya wadhamini imeongezeka kutoka wadhamini 250 hadi wadhamini 450 huku idadi ya mikoa nayo ikiongezeka kutoka 10 hadi 15.
Nape amesema kuongeza kwa wadhamini hao ni kutokana na idadi ya wanachama wao kuongezeka na wakati huo huo mikoa nayo imeongezeka.Hivyo lazima wagombea waende kwenye mikoa hiyo ambapo mikoa 12 kwa Tanzania Bara na mikoa mitatu Zanzibar na moja ya mkoa uwe Pemba au Unguja.
Amesema moja ya sharti ni kuhakikisha wadhamini wa mgombea mmoja wa ngazi ya urais hawatakiwi kuwa wadhamini wa mgombe mwingine .Hivyo kila mdhamini mmoja anatakiwa kumdhamini mgombea mmoja na si zaidi.
“Tumekubaliana kwenye NEC mwanachama mmoja anatakiwa kumdhaminni mgombea mmoja tu.Haitaruhusiwa mwachama mmoja kuwadhamini wagombea wawili.
Pia amesema wakati wa kuchukua fomu na kurejesha ni marufuku mgombea kufanya mbwembwe za aina yoyote huku akifafanua ni muhimu wagomba kusoma kanuni na kuzielewa mapema.
Kwa mujibu wa Nape ni kwamba vikao vya uchuchaji ni kwamba Kamati ya Maadili na Usalama itachuja majina ya wagombea urais Julai 8 mwaka huu, Kamati Kuu(CCM) itachuja majina Julai 9 mwaka huu na Halmashauri Kuu nayo itapitisha jina la mgombea Urais Zanzibar.
Wakati kwa jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina litapitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Julai 11 mwaka huu mjini hapa.
Alisisitiza wagombea urais wanatakiwa kuheshimu kanuni za chama hicho katika mchakato mzima wa kuchukua fomu, kurudisha na hata wakati wa kutafuta wadhamini na mwaka huu masharti yameongezeka kidogo likiwemo la idadi ya wadhamini na wagombea kuhakikisha hawakiuki kanuni za maadili.
“Sharti ambalo limetolewa na NEC ni kwamba marufuku wajumbe wa NEC na Kamati kuu kuwadhamini wagombea urais kwani wao ndio watakaopitisha jina la mgombe, hivyo hawatakiwi kua sehemu ya wadhamini.
Kuhusu kuchukua fomu ya udiwani, ubunge na uwakilishi, Nape amesema fomu zitaanza kutotolea Julai 15 mwaka huu na kurudishwa Julai 19 mwaka huu wakati mikutano ya kempeni itaanza Julai 20 hadi Julai 31 mwaka huu.
Nape alisema kura ya maoni itafanyika Agosti 1 mwaka huu wakati wabunge wa viti maalumu nayo itakuwa Julai 15 mwaka huu na kurudisha fomu Julai 19 na kufafanua uchujaji wa majina utafanywa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake(UWT), Taifa licha ya kwamba mchakato wake utapita Baraza la Vijana.
Kwa upande wa gharama za fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chama hicho,Nape alisema fomu ya kugombea urais itakuwa sh.milioni moja, wakati fomu ya kugombea ubunge ni sh.100,000 na fomu ya udiwani sh.50,000

No comments:

Post a Comment

Maoni yako