Shirika la ndege la Etihad Airways (http://www.etihad.com) ni shirika la ndege la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu, ambalo linatarajia kuongeza safari zake barani Afrika kwa kuzindua safari mpya ya kila siku Mjini Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi Tanzania.
Safari hizi za ndege kati ya Abu Dhabi na Dar es Salaam, zitaanza tarehe 1 mwezi Desemba 2015, zikiendeshwa kwa kutumia ndege ya Airbus A320 yenye viti 16 vya kitengo cha Biashara na 120 vya kitengo cha Uchumi.
Dar es Salaam itakuwa kituo cha 110 cha Etihad Airways duniani kote, na kituo cha 11 barani Afrika na Bahari ya Hindi. Ratiba hii ya kila siku itatoa njia mbili za uunganishwaji katika kitovu cha Etihad Airways mjini Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji rahisi wa safari zingine za vituo 45 maarufu katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Bara Dogo la India, Asia Kaskazini na Kusini-Mashariki, na Australia