FIFA imemchagua tena Mhe.Sepp Blatter kuwa Rais wa FIFA baada ya mpinzani wake Prince Ali kujiengua dakika za mwisho. Blatter anaishika nafasi hiyo kwa mara ya Tano mfululizo tangu aingie katika ngazi hiyo ya Uongozi mwaka 1998.
Sepp Blatter ametangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Shirikisho la Soka Duniaani FIFA kwa mara ya 5 mfululizo baada ya kupata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa msindi, Blatter amesema anajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo kuanzishwa kwa mchezo wa soka la ufukweni (Beach Soccer).
“Tumefanikiwa kuanzisha Beach Soccer na sasa mchezo huo unachezwa kote duniani”
Akizungumzia umri wake, Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa umri mkubwa hauwezi kumzuia mtu kutimiza majukumu yake, na hivyo kwake umri siyo tatizo.
Tanzania imewakilishwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi ambaye tayari alikwisha tangaza msimamo wa Tanzania kuwa ina muunga mkono Sepp Blatter, kwa maana hiyo bila shaka kura yake ni miongoni mwa kura 133 alizopata Blatter.
Kwa upande wa mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein amekubali matokeo na kutangaza kujitoa baada ya awamu ya kwanza ya upigaji kura
Friday, 29 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako