Moshi ukifuka eneo la tukio Usafiri kutoka na kwenda Mbagala ulikuwa ni kwa MIGUU (TZ 11) Wananchi wakiagizwa waondoke eneo hilo maana si salama kutokana na mabomu hayo Wanajeshi wakiondoa mabaki ya mabomu hayo. Bomu
Katika mfululizo huu ninawaletea picha za fedha za nyumbani Tanzania katika nyakati tofauti tofauti za uongozi tangu zamani hadi sasa. Hii ni katika kujikumbusha tu fedha tulizowahi kutumia.
Picha zote kwa hisani ya www.banknotesinfo.com/Tanzania
Shilingi Elfu Kumi hadi sasa Shilingi Elfu Kumi wakati wa Mwinyi Shilingi 5000-hadi sasa Shilingi Elfu Tano wakati wa Mkapa Shilingi Elfu Tano wakati wa Mwinyi Shilingi 2000-hadi sasa Shilingi 1000-hadi sasa Shilingi 1000-Mkapa Shilingi 1000-Mwinyi
Shilingi 1000-Nyerere Shilingi 500 toka wakati wa Mhe.Mkapa hadi sasa Shilingi 500 wakati wa Alhaji Mwinyi Shilingi 200 wakati wa Alhaji Mwinyi Shilingi 100 nyakati za mwanzo za Nyerere Shilingi 50 wakati wa Mwinyi
Shilingi Hamsini wakati wa Nyerere Shilingi 20 wakati wa Mwinyi Shilingi 20 wakati wa Nyerere
Shilingi 10 wakati wa Nyerere Shilingi 5 nyakati za mwanzo wa Nyerere
Mtoto mzuri wa nyumbani akitazama uchochoro wa kuelekea nyumbani,huku mazingira yakionekana yenye uhai kwa kijani kibichi.Kweli nyumbani kuzuri licha ya mambo ya DECI na EPA.
Mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi ndugu FAUSTINE KABUYE alifariki katika ajali hiyo pamoja na watu wengine wawili sehemu za Kilosa mkoani Morogoro
Leo ni sikukuu muhimu sana katika historia ya nchi yetu ambapo Tanganyika na Zanzibari ziliunganishwa na kuwa TANZANIA.Twajivunia Muungano wetu, matunda na Hayati Mwl.Nyerere na Hayati Mzee Karume. Tuudumishe muungano.Mungu Ibariki Tanzania.
Wakati hali ya maisha inazidi kuwa ngumu,baadhi ya watu wanaendelea kujiwajibisha ili kujikimu kimaisha, lakini wengine wanaona bora wakae barabarani na kuomba msaada kwa wapita njia. Yaani ni kama vile huyu kaka anayewajibika kupasua mawe kupata kokoto anapoziuza, akiwa anarudi nyumbani apitie hapo alipokaa huyu mama ombaomba ampatie kiasi kidogo, hii si sawa jamani. Tuendelee kuwajibika tu maisha yataboreka.
"DON'T JUST SIT THERE, DO SOMETHING" lakini hiyo "SOMETHING" isiwe kuombaomba
Mkojo wa ng'ombe unapotumika badala ya maji Wengine hapa wanayachezea maji Ukame unaosababishwa na kukosekana kwa mvua ya kutosha kumefanya mito,vijito,visima na mifereji kukauka. Maji yamekuwa shida na hivyo kuwafanya wenzetu watafute mbinu mbadala ya kupata kimiminika kama maji.
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!