Taswira ya Tazara Flyover
Waziri wa Ujenzi Dk,John Magufuli jana ametia saini na mkandarasi wa Japani tayari kwa kuanza ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Dkt,Magufuli akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam hususani Jimbo la Ukonga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Moshibar Mombasa, katika wilayan ya Ilala alisema kuwa baada ya kuunganisha ujenzi wa barabara za mikoa na Wilaya sasa nguvu zake zinaelekeza kukabiliana na mkakati wa kuondoa foleni.
Alisema kuwa katika kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo katika jiji la Dar Salaam juhudi za kujenga barabara za juu zinaendelea na tayari Serikali imeshapata fedha ambazo zitajenga barabara hiyo (flyover) kwenye makutano ya ya mataa ya Tazara.
Akitoa ufafanuzi huo kwa wananchi ambao walijitokeza kwa wingi katika mkutano wake alisema kuwa (jana ) yaani juzi amesaini mkataba wa kuaza ujenzi wa barabara hiyo ya njia saba, ambapo kukamilika kwake kutasaidia kupunguza tatizo la foleni.
“Nakwenda kusaini mkataba wa kuanza ujenzi wa (flyover) kwenye makutano ya tazara,na fedha zimekwishaingia mkandalasi ameshapatikana wa Japani tayari kuaza ujenzi wa barabara hiyo.”alisema.
Aliongeza kuwa mbali na eneo hilo la Tazara pia Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze kwa sh.trioni 2.4 na daraja kubwa kutoka Salenda bridge kuzunguka Cocobeach zaidi ya bilioni 200,zimeshapatikana.
Aidha alisema daraja la kigamboni mita 60 linatarajia kukamilika muda mfupi ujao hivyo likisha kamilika na kukamilika kwa njia hizo kwa kiasi kikubwa kutamaliza foleni jiji la Dar es Salaam
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan imewekeana saini mkataba wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa maradi wa barabara ya juu(Flyover) katika makutano ya barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Nafasi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Mhe. Dkt. John Magufuli ameeleza kuwa fedha hizo zinatokana na msaada wa shilingi bilioni 93.438 kutoka Serikali ya Japan huku na shilingi bilioni 8.26 zikichangiwa na Serikali ya Tanzania.
Mhe.Dkt. Magufuli aliongeza kuwa hatua hii ya uwekaji saini ni faraja kubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwa mradi huu wa ujenzi wa flyover utasaidia katika kupunguza kero ya msongamano wa magari jijini.
“Hatua hii ni nzuri na ya faraja kwa wananchi wa Tanzania itakayosaidia kupunguza kero ya msongamano wa magari na hivyo kurahisisha usafiri na kuondpkana na kero ya msongamano”alisema Mhe.Dkt Magufuli
Aidha aliongeza kuwa Serikali ya Japan imekuwa ikishirikiana kwa karibu sana na Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya barabara na madaraja ikiwemo barabara ya Mwenge kwenda Tegeta mradi uliogharimu bilioni 88,Mwenge kwenda Morocco ambayo ipo katika mkakati ,pamoja na mradi wa flyover wa Mbagala Rangi tatu kwenda Tazara.
Pia Mhe.Dkt. Magufuli alieleza kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha inawaunganisha wananchi wake kupitia mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano na usafirishaji wa watu ,bidhaa na biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi. Patrick Mfugale ameelezwa kufurahishwa na hatua hii ikiwa ishara na mwanzo wa kuleta maendeleao kwa wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisubiria kwa muda kuanz wa kwa mradi huu wa flyover ya Tazara.
Alizidi kubainisha kuwa ujenzi wa mradi huo utafanywa na mkandarasi kutoka kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction kutoka nchini Japan na utachukuwa muda wa miezi 35 kukamilka ikifuatiwa na kipindi cha uangalizi kwa muda wa miezi 12 sawa na mwaka mmoja.
Kwa Upande wa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amesema kuwa uhusiano wa Tanzani na Japan ni wa muda mrefu na kupitia mradi huu wa Flyover ya Tazara ni kielezo tosha cha kuendelea kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili utakaowasaidia kuwaletea maendeleo kwa wananchi wa Tanzania pamajo na kukuza uchumi wa nchi na nchi jirani.
Friday, 16 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako