BAADA ya kufika kwa gesi asilia jijini Dar es Salaam ikitokea Mtwara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), itaingiza gesi hiyo katika mitambo yote ya umeme nchini, hivyo kuanzia leo kutakuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa.
Akizungumza katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi One jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo hicho kikubwa.
“Wiki hii umeme utakatika sana kutokana na kuunganishwa gesi kutoka Mtwara kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kuanzia kesho mitambo yote itazimwa,” alisema Mramba.
Monday, 7 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako