Sunday, 28 June 2009
USAFIRI WA NYUMBANI
Hii ni Nzega Tabora.Usafiri kama huu ni tangu mababu. Kuna haja ya kubadili jamani, maana hata kwa namna fulani haki za wanyama zinakiukwa hapa.
Hii ni "enzi za mwalimu" ambapo Basi kama hili lilitumia siku 3 njiani kutoka sehemu moja hadi nyingine fupi tu.
Leo tuna usafiri huu murua,Kutoka Dar hadi Arusha huku ukijisomea gazeti na soda pembeni, muziki mwanana, full kipupwe n.k.
Baada ya muda tutarajie na haya nayo yaja kwa usafiri wa Ferry - Kigamboni na Mwanza City - Ukerewe hahahahaha
Ila kwa wakati huo huo , kuna huu usafiri mwingine tena unaokuja kwa kasi sana hasa Jijini Dar, sijui ndio ubunifu au....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ama kweli kuna mengi ambayo serikali inastahili kuwaeleza wananchi juu ya nini wamefanya, wanafanya na watafanya kuondokana na usafiri huu ambao haustahili kuwa ndio tegemezi kwa wengi.
ReplyDeleteAsante Mkuu
Kweli kabisa inabidi serikali ifanye kazi yake kwani kuna magari yapo na yanaoza bure na wengine wanapata taabu. Kazi kwelikweli.Jumapili njema.
ReplyDeleteAsanteni kwa maoni mazuri,yananipa moyo. Nanyi hongereni pia kwa kazi nzuri.
ReplyDelete