Saturday, 20 June 2009

NJAA KATIKA NCHI YENYE SHIBE

Nimetumia msemo huu "Njaa katika nchi yenye shibe" nikiwa na maana ya hali ya nchi ya Tanzania, kwamba imebarikiwa maliasili nyingi ambazo kama zinatumiwa ipasavyo, "njaa" kwetu ingekuwa msamiati. Hii inanikumbusha moja ya mabango niliyoyaona katika pitapita zangu nchini Uingereza wanavyopambana na njaa,linasomeka "MAKE POVERTY HISTORY" yaani Fanya njaa iwe historia. Nasi tungeweka kauli mbiu hii na kuifanyia kazi.

IDADI ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula nchini, imeongezeka kutoka 240,500Januari mwaka huu,hadi kufikia 780,416 mwezi huu.
Katika ziara ya Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo, Januari mwaka huu kwenye Kitengo cha Hifadhi ya Chakula, ilibainika kuwa mikoa yenye wilaya 20, ilikuwa inahitaji tani 7,782 za chakula, kwa ajili ya watu wanaokabiliwa na tatizo hilo.

Hata hivyo imebainika kuwa idadi ya watu wanaohitaji chakula cha haraka katika kipindi cha kati ya mwezi uliopita na Julai mwaka huu, imeongezeka mara tatu zaidi.
Akizungumza na Mwananchi jana, Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Richard Kasuga, alisema,tathmini ya Aprili mwaka huu, ilionyesha kuwa watu bado kuna tatizo la upungufu wa chakula licha ya baadhi ya maeneo kupata mavuno ya kuridhisha.

"Tathmini ya mwezi Aprili mwaka huu inaonyesha kuwa jumla ya watu 780,416 wanakabiliwa na upungufu wa chakula,"alisema Kasuga.
Alisema jumla ya tani 28,095 za chakula zitahitajika kwa ajili ya watu hao wa maeneo mbalimbali nchini.
Kulingana na taarifa ya awali, baadhi ya mikoa ambayo watu wake wanakabiliwa na tatizo hilo ni Singida, Arusha, Morogoro, Mwanza, Dodoma, Shinyanga, Lindi, Tabora, Mtwara, Kilimanjaro,na Pwani.
Wilaya 36 za mikoa hiyo, ndizo zinazokabiliwa na tatizo hilo.

NA HAYA NDIO MADHARA YAKE

Wanafunzi wa darasa la 5 na la sita wa shule ya msingi Mulungu wilayani Mbarari mkoani Mbeya wakiwa wanatumia darasa moja kupigia buku kufuatia uhaba wa madarasa shuleni hapo


Watoto wadogo wakifanya biashara badala ya kwenda shule au kuwa nyumbani na wazazi wakiwasaidia kazi za nyumbani,sio hizi.
Kukosa hela za kulipa nauli kunapelekea wanafunzi kuhatarisha maisha kwa kudandia magari haya kupata "lift"
Mwanafunzi kushindia kikombe kimoja kidogo cha uji siku nzima, na wakati huo huo asome na kufaulu (wapi na wapi!!!!)
Njaa inapouma hata darasani hakukaliki labda kulalika tu, na mitihani ikija ufaulu pia

No comments:

Post a Comment

Maoni yako