Tatizo ni kiasi. Nadhani ni vema kwa hawa kujifunza shughuli kama hizo, lakini WAFUNZWE na sio KUADHIBIWA. Wakibebeshwa kikuni kimojakimoja ama kukopo ka maji badala ya fungu zima la kuni na dumu la maji watajifunza. Hivi ni vitu ambavyo tunatakiwa kuwafunza. Wanatakiwa kujua ratiba ya maisha ya ndani na hata kuona mahangaiko na mkanganyiko wa maisha ambao wazazi wanapitia kuwafikisha walipo wao. Tatizo linakuja pale ambapo watoto wanatumika kama sehemu ya "nguvukazi" na kupangiwa mzigo sawa na mtu mzima na matokeo yake kwa kuwa hawawezi kuubeba kwa wakati mmoja, wanalazimika kurejea tena na tena na tena kubeba kidogokidogo na hapo wanaanza kuiona hiyo kama ADHABU badala ya ELIMU YA MAISHA. Kwa hiyo nadhani mzigo ukipungua na wao wakaoneshwa namna ya kufanya, watapenda na hilo ni la kusisitiza. Blessings
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!
Tatizo ni kiasi. Nadhani ni vema kwa hawa kujifunza shughuli kama hizo, lakini WAFUNZWE na sio KUADHIBIWA. Wakibebeshwa kikuni kimojakimoja ama kukopo ka maji badala ya fungu zima la kuni na dumu la maji watajifunza. Hivi ni vitu ambavyo tunatakiwa kuwafunza. Wanatakiwa kujua ratiba ya maisha ya ndani na hata kuona mahangaiko na mkanganyiko wa maisha ambao wazazi wanapitia kuwafikisha walipo wao.
ReplyDeleteTatizo linakuja pale ambapo watoto wanatumika kama sehemu ya "nguvukazi" na kupangiwa mzigo sawa na mtu mzima na matokeo yake kwa kuwa hawawezi kuubeba kwa wakati mmoja, wanalazimika kurejea tena na tena na tena kubeba kidogokidogo na hapo wanaanza kuiona hiyo kama ADHABU badala ya ELIMU YA MAISHA.
Kwa hiyo nadhani mzigo ukipungua na wao wakaoneshwa namna ya kufanya, watapenda na hilo ni la kusisitiza.
Blessings
Ni kweli Mzee wa Changamoto. Asante kwa mchango wa mawazo.
ReplyDelete