Picha hii haihusiani na taarifa yenyewe bali ni kiwakilisho tu kuipa nakshi habari
Na Aziza Nangwa
Vituo vitano vya mafuta vimetozwa faini mkoani Ilala kwa makosa ya udanganyifu kwa wateja wanaokwenda kujaza mafuta kwenye vituo hivyo.
Akizungumza na mwananchi ofisini kwake jana meneja wa wakala wa vipimo mkoani Ilala Agustino Maziku, alisema baada ya kukagua vituo 60 vilivyopo mkoani Ilala na waligundua vituo vitano vya mafuta vikikiuka sheria za vipimo kwa kutoa rakiri katika mashine za kupimia mafuta.
Maziku alifanunua kwamba vituo vyote vya mafuta vinakuwa na mashine ambazo ni seals ambazo husaidia mashine hizo kupima mafuta kwa haki bila ya kumpunja mteja lakini zikichezewa huwa na uwezo wa kubadilisha mita za pampu ziweze kutoa mafuta kidogo na huku zikionyesha zimetoa mafuta mengi hivyo kumsababishia mteja asipate kiasi cha mafuta aliyokusudia bila yeye kujua.
“Lazima watu wote wajue sisi kazi yetu ni kusimamia swala zima la kuhakikisha vipimo vinakwenda sawa. Tunahakikisha watu hawapunjani sehemu zote hata kwenye vifungashio vya viwandani wanapima idadi sahihi iliyoandikwa kwenye kifungashio hicho”alisema Maziku
Alisema kuwa sambamba na operesheni hiyo walifanikiwa kamata watu 152 kwenye vizuizi vyao mbalimbali kwa kukiuka ufungashaji bidhaa kwa kutumia kipimo cha lumbesa badala ya ufungaji wa kawaida na waliwatoza faini kila mmoja.
Maziku alisema wamekuwa wakifanya msako wa namna hiyo mara kwa mara kulingana na hali halisi iliyopo na kuwa wamekuwa wakikagua kipimo kimoja kimoja na kutoa taarifa maalumu inayowataka wateja wa eneo husika kuleta mizani yao katika ofisi za watendaji ili vipitiwe na kwamba mtaalamu wa vipimo na anayekiuka anatozwa faini.
Katika operesheni yetu ya hivi karibuni tumekamata jumla ya mizani feki 30 na zingine 24 zilizochezewa ili zisitoe vipimo sahihi 24.
Hata hivyo Maziku alisema changamoto zinazowakabili kwa sasa ni upungufu wa watumishi, vyombo vya usafiri na gharama za uendeshaji zoezi katika idara yake havitoshi kulingana na eneo, magari yaliyopo hayatoshi kwenda kwenye maeneo haraka zaidi.
Pia aliwataka wananchi wenye nia njema washirikiane na ofisi yake ya vipimo kutoa taarifa mara kwa mara pale wanapoona kuna ubabaishaji katika vipimo kwenye maeneo yao.
Monday, 22 June 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako