Mh.Paul Makonda akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi anasema tarehe 5/1/2016 ujenzi wa shule 7 katika wilaya ya kinondoni ulianza na amezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa shule Saba za kata katika wilaya ya Kinondoni ili kupunguza upungufu wa shule katika wilaya hio ambapo zitachukua zaidi ya vijana 3183
Akiongelea maendeleo ya Kampeni hio amesema inaenda vizuri na michango inaendelea kumfikia na witikio umekuwa mkubwa sana!
Akitoa tathimini fupi amesema amepokea Mifuko 500 ya cement toka kwa Dr mwaka....mifuko 1000 ya cement toka kwa watu mbalimbali na umoja wa mafundi geleji wametoa mifuko 50 ya cement! Amesema ameamua kujenga shule hizo saba kuondokana na tatizo la upungufu wa shule katika wilaya ya kinondoni na kuongeza kuwa Elimu ni njia bora na pekee ya kuwapa urithi wadogo zetu na watoto zetu! Ameendelea kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia kwani Kutoa ni moyo na si utajiri ameomba mwenye chochote hata mfuko mmoja wa simenti iwe hata tofari moja au mawe na mchanga wanapokea chochote
MAONI YANGU!
Mh.Paul Makonda ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote hapa nchini katika utendaji wa kazi,Hata wabunge pia ni lazima wajifunze toka kwa Makonda na si kubaki kuilalamikia serikali inafanya nini ni wakati wa wao pia kusema serikali wameifanyia nini
Ukiacha maneno yanayo semwa kuhusu Mh.Paul Makonda utendaji wake wa kazi wananchi wengu wameupenda pamoja na mapungufu machache alio nayo
Saturday, 16 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako