Wednesday, 17 June 2015

TCRA YAZINDUA MFUMO MPYA WA KUSAJILI NA KUHAKIKI NAMBA ZA SIMU

Mfumo mpya wa Usajili wa Namba za Simu (Sim Card registration) kwa kutumia Teknolojia mpya ya Kidigitali Kupitia Smart Phone kwa Programu ya KYC umezinduliwa Rasmi leo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukiwahusisha Makampuni ya simu, NIDA, Polisi na TCRA.
Akizungumza katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma hiyo ya kisasa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema kuwa mwanzo kulikuwa hakuna changamoto sana juu ya laini za Simu lakini kwa sasa zaidi ya laini za simu 32,000,000 zilizo sajiliwa, Pia alizungumzia umuhimu wa kujisajili ikiwa ni pamoja kwa usalama, kutunza amani pia kusaidia mamlaka kuwa na kumbukumbu za watu ambao wamejisajili..
Nae Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meeza alielezea kwa kina namna ya mfumo huo mpya utakavyofanya kazi ambapo katika usajili mpya wa Kielekrinki kutakuwa na kusajili kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ambapo zoezi kupata vitambulisho vya Taifa kwa wananchi Tanzania Linaendelea.
Alielezea Mfumo huo mpya wa Sim Card registration kuwa unakwenda kwenda kwa kutumia Smartphone ambayo itakuwa na Programu ya KYC ambapo mteja atasajiliwa ndani ya simu hiyo kuanzia kuandika Majina yake, Atapigwa Picha, Kitambulisho chake kitapigwa picha kama ni Feki Mashine Simu haita kipiga picha, pia Mteja ataweza kutia Saini yake pale pale kwenye simu. Aliongeza kuwa Mfumo huo utapatikana kwa Mawakala wa Makampuni husika wa Simu za mkononi. Alimalizia kwa kusema kuwa Mfumo huo mpya utatumika kwa kuanza kusajili namba mpya za simu kwa Kutumia kitambulisho cha Taifa kama ndio Kitambulisho Rasmi ingawa viambulisho vyengine kama Hati ya kusafiria itaweza kutumika, Pia mfumo huo utatumika kuhakiki Namba za simu ambazo tayari zimesajiliwa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako