SERIKALI imesema waathirika wa mafuriko ya mto Msimbazi walioondoka baada ya kupewa viwanja maeneo ya Mabwepande na kurudi eneo la Msimbazi watanyang’anywa viwanja hivyo.Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki ya upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofikia tamati leo kwa upandaji miti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mji Mpya iliyopo Mabwepande ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa mwenyeji.“Natoa maagizo kuwa wale wote waliopewa viwanja na serikali hapa Mabwepande ambao wameondoka viwanja vyao wanyang’anywe kwani ni wasariti na wale waliouziwa imekula kwao kwani serikali haiwatambui” alisema Sadiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakiserebuka pamoja na wananchi katika maadhimisho hayo ya upandaji miti mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Makonda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako