Tuesday, 30 May 2017

ALIYEBUNI NA KUCHORA NEMBO ZA TAIFA AFARIKI DUNIA


Mzee Francis Maige Kanyasu maarufu kama "Ngosha" aliyedai kuwa yeye ndiye mchoraji wa nembo ya Taifa amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, leo akiwa na umri wa miaka 86.!

Monday, 29 May 2017

UTEUZI WA IGP

Aliyekuwa Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa polisi (IGP).

Saturday, 27 May 2017

NAWATAKIA NDUGU ZETU WAISLAM MFUNGU MWEMA WA MWZI MTUKUFU WA RAMADHAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla na kuwatakia kheri katika mwezi huo,pia amewataka kujitahidi kufanya ibada kwa wingi,ikiwemo kusima Quran,kuswali sana hasa swala za Suna na kutoa zaka.

Thursday, 25 May 2017

TANZIA......MUME WA ZAMANI WA ZARI THE BOSS AFARIKI DUNIA

Marehemu Ivan Don Marehemu Mume wa zamani wa Zari, Mke wa sasa wa Diamond Platnumz.

Leo May 25, 2017 zimeripotiwa taarifa za kifo cha Ivan Semwanga “Ivan Don” mfanyabiashara maarufu kutoka nchini uganda na aliyekuwa mume wa mrembo Zari the Boss Lady, ambaye amefariki baada ya kuugua ghafla takriban wiki moja sasa.

KAULI YA BABA WA TAIFA KUHUSU MADINI

HOT NEWZ.......MHE PROFESA MUHONGO AACHISHWA UWAZIRI

IKULU: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ambapo uteuzi wa kujaza nafasi yake utafanyika baadaye.

Wednesday, 24 May 2017

BREAKING NEWZ......WATU 19 WAUAWA KATIKA TUKIO LA KIGAIDI HUKO MANCHESTER UINGEREZA

Watu 19 wameuwawa na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika tukio linashukiwa kuwa ni shambulizi la kigaidi katika ukumbi wa Manchester Arena.Mlipuko huo umetokea usiku wa jana wakati wa tamasha la muziki la mwanamuziki wa pop kutoka Marekani Ariana Grande.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa pole kwa wafiwa na waliojeruhiwa na tukio hilo ambalo polisi wanalichukulia kama shambulizi la kigaidi

MCHEZA FILAMU JAMES BOND AFARIKI DUNIA

BASATA LALAANI KITENDO CHA PICHA ZISIZO NA MAADILI ZA BEN POL

Jamii za Tanzania inabidi ifike mahali iachane na mambo ya kuiga,hasa tabia yisiyoendana na maadili ya Mtazania. Pengine wanaiga bila kujua, ila wengi wanajua wanachofanya na wakati mwingine wanafanya makusudi kwa kisingizio cha ukuaji wa Sayansi, teknolojia na Demokrasia
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha za nusu za utupu za msanii wa muziki, Ben Pol ambazo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii

Monday, 22 May 2017

MKATABA UJENYI WA BOMBA LA MAFUTA HOIMA UGANDA HADI TANGA TANZANIA WASAINIWA

Marais waheshimiwa Yoweri Museveni wa Uganda na John Magufuli wa Tanzania wakisiani Mkataba huo
Maraisi hao wakipeana mkono wa pongeyi na shukrani kwa ushirikiano huo baada za kusaini mkataba
Kikao cha majadiliano za mwisho kabla ya mkataba kusainiwa