Friday, 18 April 2014

KWA MWENDO HUU KWELI KATIBA TUTAIPATA?

WAJUMBE karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza. Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba. Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko. Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu…

No comments:

Post a Comment

Maoni yako