Saturday, 20 June 2009

PRECISION AIR YAONGEZA SAFARI KWENDA NCHI JIRANI


DAR-ENTEBBE & KIA-ENTEBBE MARA NNE KWA WIKI

Kuanzia Julai 2, 2009 siku za kusafiri kati ya Dar na Entebbe kupitia Mwanza, vilevile kutoka Kilimanjaro kwenda Entebbe kupitia Mwanza zimeongezeka na kuwa 4 kwa wiki.
Kila Jumatatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumapili ndege itaondoka Dar saa 12.00 asubuhi na kuondoka Entebbe saa 6.25 mchana kurudi Dar.
Ndege itaondoka Kilimanjaro saa 3.15 asubuhi na kuondoka Entebbe saa 6.25 mchana.

Kwa maelezo zaidi piga simu no.
+255 787 888 408/409/417 au +255 22 2168000
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano,
Precision Air

WEEKEND NA KICHEKO CHA KATUNI



NJAA KATIKA NCHI YENYE SHIBE

Nimetumia msemo huu "Njaa katika nchi yenye shibe" nikiwa na maana ya hali ya nchi ya Tanzania, kwamba imebarikiwa maliasili nyingi ambazo kama zinatumiwa ipasavyo, "njaa" kwetu ingekuwa msamiati. Hii inanikumbusha moja ya mabango niliyoyaona katika pitapita zangu nchini Uingereza wanavyopambana na njaa,linasomeka "MAKE POVERTY HISTORY" yaani Fanya njaa iwe historia. Nasi tungeweka kauli mbiu hii na kuifanyia kazi.

IDADI ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula nchini, imeongezeka kutoka 240,500Januari mwaka huu,hadi kufikia 780,416 mwezi huu.
Katika ziara ya Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo, Januari mwaka huu kwenye Kitengo cha Hifadhi ya Chakula, ilibainika kuwa mikoa yenye wilaya 20, ilikuwa inahitaji tani 7,782 za chakula, kwa ajili ya watu wanaokabiliwa na tatizo hilo.

Hata hivyo imebainika kuwa idadi ya watu wanaohitaji chakula cha haraka katika kipindi cha kati ya mwezi uliopita na Julai mwaka huu, imeongezeka mara tatu zaidi.
Akizungumza na Mwananchi jana, Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Richard Kasuga, alisema,tathmini ya Aprili mwaka huu, ilionyesha kuwa watu bado kuna tatizo la upungufu wa chakula licha ya baadhi ya maeneo kupata mavuno ya kuridhisha.

"Tathmini ya mwezi Aprili mwaka huu inaonyesha kuwa jumla ya watu 780,416 wanakabiliwa na upungufu wa chakula,"alisema Kasuga.
Alisema jumla ya tani 28,095 za chakula zitahitajika kwa ajili ya watu hao wa maeneo mbalimbali nchini.
Kulingana na taarifa ya awali, baadhi ya mikoa ambayo watu wake wanakabiliwa na tatizo hilo ni Singida, Arusha, Morogoro, Mwanza, Dodoma, Shinyanga, Lindi, Tabora, Mtwara, Kilimanjaro,na Pwani.
Wilaya 36 za mikoa hiyo, ndizo zinazokabiliwa na tatizo hilo.

NA HAYA NDIO MADHARA YAKE

Wanafunzi wa darasa la 5 na la sita wa shule ya msingi Mulungu wilayani Mbarari mkoani Mbeya wakiwa wanatumia darasa moja kupigia buku kufuatia uhaba wa madarasa shuleni hapo


Watoto wadogo wakifanya biashara badala ya kwenda shule au kuwa nyumbani na wazazi wakiwasaidia kazi za nyumbani,sio hizi.
Kukosa hela za kulipa nauli kunapelekea wanafunzi kuhatarisha maisha kwa kudandia magari haya kupata "lift"
Mwanafunzi kushindia kikombe kimoja kidogo cha uji siku nzima, na wakati huo huo asome na kufaulu (wapi na wapi!!!!)
Njaa inapouma hata darasani hakukaliki labda kulalika tu, na mitihani ikija ufaulu pia

Thursday, 18 June 2009

TOFAUTI YA "A" na "Z"

Moja ya nyumba za ghorofa za vijijini

Ghorofa za Benki Kuu Tanzania Jijini Dar-es-Salaam

Watoto wakiwa kanisani, katika moja ya makanisa ya Vijijini.
Hili nalo ni Kanisa wanakohudhuria kusali watu wengine kama wafanyavyo hao watoto hapo juu
Hali halisi ya maisha ya wototo walio wengi
Waliobahatika wachache katika nchi yenye heri

MSICHANA MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI KWA SASA

Jyoti Amge ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15, ni mrefu wa futi1 na inch 11,ndiye anayedhaniwa kuwa msichana mfupi kuliko wote duniani.Akiwa na wanadarasa wenzake shuleni
Hapa akiwa na dada zake Rupali(18), Archana(23), Mama yake Ranjana Amge(45), Baba yake Kishan (52), na kaka yake Satish(22)

"VIJIMAMBO NDANI YA NDOA"


SULUHISHO LA UKIMYA

Mume na mke wake walikuwa na malumbano nyumbani wakaamua kunyamaziana kama suluhisho(silent treatment)
Mara mume alihamaki na kugundua kuwa itabidi amuombe mke wake amuamshe mapema alifajiri saa 11 ili aweze kuwahi ndege kwa ajili ya safari zake za kibiashara.Ila kwakuwa hakutaka kuwa wa kwanza kuvunja ukimya na hivyo kupoteza msimamo, aliamua kuandika ujumbe katika kipande cha karatasi ukisema "TAFADHALI NAOMBA NIAMSHE SAA 11 ALFAJIRI" Akaiweka mahali alipojua itakuwa rahisi mkewe kuiona, kisha akalala.
Asubuhi yake aliamka akijikuta amechelewa maana ilikuwa ni saa 3asubuhi. Akiwa amekasirika sana akitaka kumfuata mkewe na kumfokea kwa kutokumuamsha alivyoomba, akahamaki kuona kipande cha karatasi karibu na kitanda chake kimeandikwa " NI SAA 11 ASUBUHI SASA, AMKA MUME WANGU"
Tunajifunza nini hapa?????????????????????????????

TUJIKUMBUSHE HAYA......



NGUZO TANO ZA UJAMAA - KWA MUJIBU WA JULIUS K. NYERERE, SABA SABA 1970

1. 'WATU WOTE NI SAWA'"...

Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza... mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere
2. 'LAZIMA MTU AFANYE KAZI'

"...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

3. 'HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU'"...


Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanye kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama... ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere




4. 'VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA'




"...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere




5. 'KUUNDA NCHI BILA MATABAKA'


"..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. NyerereNUKUU ZIMETOKA KWENYE UJAMAA NI IMANI: MOYO KABLA YA SILAHA, 1973: EAPH

Wednesday, 17 June 2009

UJUAJI MWINGINE!!!!!

Hapa jamaa anajiona amejilinda na ajali.

MISHKAKI

Raha ya kuwa nyumbani ni kupata mishkaki saaafi

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Jana ilikuwa siku ya Mtoto wa Afrika.Tunapata changamoto gani kwa kuadhimisha siku hiyo?
Watoto waliopoteza wazazi wao kutokana na matatizo mbali mbali wa kituo cha Tanzania Mitindo House. Kilicho chini ya mpiganaji Khadija Mwanamboka Saad. Katika picha ya pamoja ikiwa ni siku ya kimataifa ya mtoto wa Afrika.Miss Earth, Evelyene na Miss International, Hidaya Maeda, wakipiga picha ya pamoja na watoto wa shule ya Malaika Montessori.
Picha kwa hisani ya Global Publishers