Wednesday, 18 December 2013

Sudan Kusini hali si shwari

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba. Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer. Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo. Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao. Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako