Saturday, 11 April 2009
WATOTO WA MARAISI WA ZAMANI (TANZANIA & UGANDA)
WATOTO wawili wa viongozi wa zamani wa Uganda na Tanzania jana waliandika historia mpya baada ya kukutana kwenye kijiji cha Butiama alikozaliwa na kuzikwa Rais Julius Nyerere na kukubaliana kuanza umoja mpya.
Watoto hao, Madaraka Nyerere kulia na Jaffar Amin, ambao baba zao walionekana kuwa mahasimu wakubwa katika vita vya mwaka 1978 baina ya nchi hizo mbili, walionyesha kusikitikia vita hiyo, huku mtoto wa Idd Amin wa Uganda akisema "ilisababisha maafa makubwa" kwa wananchi wa Tanzania na Uganda.
"Vita ile ilisababisha maafa makubwa kwa wananchi," alisema Jaffar akionekana kusikitikia kitendo cha baba yake ambaye alikuwa chanzo cha vita hiyo kwa kuishambulia Tanzania kabla ya Nyerere kuamua kujibu mapigo kwa kuiondoa serikali yake madarakani.
habari na picha kwa msaada wa Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako