Thursday, 21 January 2016

ADHA YA MVUA JIJINI DAR

MFANYAKAZI: samahani Boss leo sitaweza kuja kazini maana ninapoishi maji yamejaa kila mahala hakuna pa kupita. Nipo kama kisiwani hapa.
BOSS: Nakumbuka ulipokuwa unaomba kazi uliorodhesha moja ya vitu unavyopendelea (Hobby) ni kuogelea. "Tukutane kazini"
Hakuna namna itabidi kutumia mbinu hii kufika kazini. Umesahau kauli mbiu ni "HAPA KAZI TU"

DKT.MAGUFULI: RAIS WA MANENO NA VITENDO

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016

Wednesday, 20 January 2016

BODABODA: HII SASA MMEPITILIZA

Linapokuja suala la usafiri wa haraka na uhakika,bodaboda zimekuwa na mchango mkubwa sana, ila kwasasa ukiukwaji wa sheria hasa usalama limekuwa kubwa. Ni muhimu kuzingatia usalama wa abiria kwa vigezo vilivyoweka mfano kuvaa Helmet, kupatia abiria mmoja tu kwa wakati mmoja, mwendo kasi....
KATIKA kukabiliana na madereva wa pikipiki wanaopakia abiria zaidi ya mmoja maarufu mshikaki, Jeshi la Polisi mkoani Pwani litatumia mbinu mpya ya kuwapiga picha madereva hao na kuwakamata baadaye wakiwa kwenye vituo vyao.

Jeshi hilo litatumia mbinu hiyo ili kuepusha ukamataji kwa kuwakimbiza wale wanaofanya hivyo kwa lengo la kuepuka kusababisha ajali wakati wa kuwakamata madereva hao wanaobeba mshikaki.

PATA UMBEA KIDOGO

Wizi mtupu............................

MWANAMAMA KATIKA UBUNIFU

Tuesday, 19 January 2016

KAMPUNI YA KONYAGI YAFANYA TAMASHA LA KUONJA WINE INAZOTENGENEZA

Kampuni ya Konyagi ambayo ni kampuni tanzu ya TBL Group hivi karibuni iliandaa tamasha la kuonja vinywaji vya wine vinavyotengenezwa na kampuni hiyo yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo lilolofanyika katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam lilikuwa kivutio kwa watu wengi na walouhudhuria kwani walipata burudani za kila aina na kufurahia ubora wa vinywaji vya kampuni hiyo bila kusahau kucheza muziki,kupata maakuli na kujishindia zawadi mbalimbali.

KASI YA MHE RAIS MAGUFULI YAANZA KUGUSA MAISHA YA NYUMBANI

Kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wamejijengea hali fulani ya maisha bila misingi imara,hali imeanza kugeuka.

Monday, 18 January 2016

TANZIA: MWANDISHI WA KITABU CHA NGOSWE

mwandishi, muigizaji na mhadhiri wa chuo kikuu cha Daresalaam na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa vitabu nchini (UWAVITA ), Edwin Semzaba. amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam

Moja kati ya kazi alizofanya enzi ya uhai wake ni kitabu cha "Ngoswe Penzi kitovu cha uzembe".
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen

Sunday, 17 January 2016

TCRA WATUMBUA MAJIPU VITUO VYA REDIO NA TV

Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..

Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.

Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.

Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.

==> Vituo vingine vilivyofungiwa ni;
Sibuka FMBreez FMCountry FMEbony FMHot FMImpact FMIringa Municipal TVKiss FMKitulo FMKifimbo FMMbeya City Municipal TVRadio 5Radio Free Afrika (RFA)Musa Television NetworkPride FM radioRadio HurumaRadio UhuruStar TVRock FM RadioStandard FM radioSumbawanga Municipal TVTanga City TVTop Radio FM limitedUlanga FM

Saturday, 16 January 2016

MEYA WAPYA KINONDONI NA ILALA DAR WAPATIKANA

Wafuasi wa Ukawa wakimpongeza Boniface Jacob (aliyesimama mbele) baada ya kushinda umeya wa Kinondoni.
Hatimaye leo uchaguzi wa meya wa halmashauri wa Kinondoni jijini Dar es Salaam umefanyika ambapo diwani wa Ubungo kutoka UKAWA, Boniface Jacob (CHADEMA) amekuwa meya na na Naibu Meya ni diwani wa Tandale, Jumanne Amir Mbunju (CUF).
Katika uchaguzi huo, Chadema kilipata kura 38 na CCM kura 20 ambapo katika unaibu meya Cuf kilipata kura 38 na CCM kura 20
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (katikati) akiongoza sala ya kufungua mkutano wa kwanza baada ya uchaguzi wa kumchagua Meya na Naibu Meya wa manispaa hiyo
Meya Mpya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kwiyeko (UKAWA)
Naibu Meya wa Ilala Mhe.Omary Salum Kumbilamoto (UKAWA)