Sunday, 20 September 2015

HUYU NDIO "TIFFAH" MTOTO WA DIAMOND NA ZARI

Baada ya kutimiza siku 40, hatimae sura ya mtoto wa Diamond yawekwa hadharani.
Diamond asema........Huyu Ndio Binti yangu...Latiffah Binti Nasibu Abdul almaaruf kama @princess_tiffah ...
Kila mmoja wetu anaweza kumfungulia mwanae NMB Junior Account na kumuifadhia fedha kwa ajili ya masomo na mahitaji yake ya baadae. Furahia usalama wa fedha zako na riba ya kuvutia! Wapigie 0800112233 kwa maelezo zaidi au tembelea tawi lolote la NMB lililo karibu yako. Follow @nmbtanzania na Facebook page ya NMB Tanzania ‪#‎NMBJUNIORACCOUNT‬
Yanayojiri nyumbani kwa Diamond huko Mdale jijini Dar katika 40 ya kuzaliwa kwa Tiffah

MHE.LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA BUKOBA

Hapa wananchi wanaitikia "MABADILIKOOOO....LOWASSAAAA, LOWASAAAA....MABADILIKO"
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi Bukoba waliofika kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.

VIDEO: DKT.MAGUFULI ALIPOHUTUBIA BIHARAMULO

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO WA RAIS WA MAREKANI MHE. BARACK OBAMA

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015
Mhe. Wilson Masilingi Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015. Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi,Mke wa Balozi.
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.

Saturday, 19 September 2015

KUJITAMBUA MUHIMU

unapokuwa uanshabikia kitu fulani na kupewa bango inabidi usome maneno hayo kabla hujaonyesha watu vinginevyo unakuwa haueleweki. Hii ilitokea Bagamoyo.

UTUNDU WA WATOTO

Umemuacha nyumbani dakika chache unarudi na kumkuta kabandua laptop hivi...!!!
UTAMFANYAJE...!!!!?

DKT MAGUFULI AHANI MSIBA WA MWALIMU WAKE WA SHULE YA MSINGI(maelezo,picha na video)

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimfariji mama Paskazia Mufuruki mjane wa Marehemu mwalimu Colner Pastor wakati alipohani msiba huo katika kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo

WANANCHI WAASWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA DART

Muonekano wa kituo cha kimara
Na Ally Daud- MAELEZO.

Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam (DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.
Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.
“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.
Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.
Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden Dragon kutoka Japan
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.

Friday, 18 September 2015

UNAZITAFSIRIJE PICHA HIZI ZA WAGOMBEA URAISI?

Mhe. Edward Lowassa
Mhe. John Magufuli

GEITA YAMPOKEA VIZURI MGOMBEA MWENZA UKAWA

Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwasili katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita jana .
Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita