Mungu ametuumba alivyotaka mwenyewe. Pia kagawa riziki kwa kila mmoja kwa namna alivyotaka. Ila busara ya kawaida inatukumbusha kuwa na matumizi mazuri kwa tulichopewa na mungu. Hapa nakupa mifano michache;
Unapokula mpaka kusaza na kuamua kumwaga jalalani, kumbuka pia kuna binadamu anakufa njaa mahali fulani. Hivyo:Tumia kwa busara Unapowaza kuchoma nguo yako moto eti kwasababu tu dobi au mfanyakazi wako hakuinyoosha vizuri........ .....Kumbuka kuna binadamu mahali fulani anatembea uchi au na nguo zilizotatuka. Hivyo: Tumia kwa busara. Au hivi na anamtukuza muumba wake. Unapowaza kutupa jalalani kiatu chako eti kwa kuwa mpiga rangi hakukingarisha vizuri...... Kumbuka kuna binadamu mwenzio anaridhika na hiki alichovaa. Au hivi tangu utotoni. Unapowaza kukataa kwenda shule kisa wazazi hawajakununulia baiskeli kama ya John..... Kumbuka kuna wanafunzi wenzio hutembea umbali mrefu kwa miguu kwenda na kurudi shule Na tena kama hiyo hatoshi,wanawasili kwenye shule yao hii hapaTuesday, 14 January 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hakika hili bi bonge la somo na wengi wetu huwa tunasahau kabisa kufikiri hivi. Ahsante kwa kutukumbusha kaka Nicky.
ReplyDelete