Monday, 12 September 2016

EID MUBARAK

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hutuba katika swala ya Idd El Haji iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi

Sunday, 11 September 2016

WAISLAM ZAIDI YA MILIONI MOJA NA NUSU WAANZA IBADA YA HIJJA HUKO SAUDI ARABIA

Ibada ya Hijja ya kila mwaka inayotekelezwa na Waislamu imeanza Jumamosi (10.09.2016) nchini Saudi Arabia huku hatua kali za kiusalama zikiwa zimeimarishwa kwa takriban mahujaji milioni 1.5 wanaoshiriki hija hiyo.
Baada ya kufanyika kwa taratibu za awali za ibada hiyo katika Msikiti Mkuu katika mji wa Mecca eneo takatifu kabisa kwa Waislamu duniani mahujaji hao Jumamosi wameanza kuelekea eneo la tambarare la Mina lilioko kama kilomita tano mashariki ya Meccca kwa kutumia vyombo mbali mbali vya usafiri na hata kwa miguu chini ya hali ya joto inayopindukia nyuzi joto 40.

Mahujaji hao watakuwa wanafuata nyayo za Mtume Muhammad (SAW) aliyefanya utaratibu huo huo wa ibada miaka 1,400 iliopita.Mamia kwa maelfu ya mahujaji wakiwa katika mavazi yao meupe yasiokuwa na mishono walianza kuondoka mji mtakatifu wa Mecca Jumamosi alfajiri kwa safari yao hiyo ya Mina ambapo watalala huko na watakamilisha hijja kwa kwenda kusimama kwenye mlima Arafat hapo Jumapili.
Tarehe 24 Septemba mwaka jana Mina palikuwa ndio mahala kulikotokea maafa mabaya kabisa katika historia ya hija kutokana na mkanyagano wakati mahujaji walipokuwa wakielekea kwenye Daraja la Jabarat kwa ajili ya kumpiga mawe shetani. Mwaka huu kumpiga mawe shetani kutaanza Jumatatu.

TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA

Saturday, 10 September 2016

TERMINAL 3 J.K NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT KATIKA PICHA

Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi.

Thursday, 8 September 2016

"SINA MPANGO WA KUHAMA CHAMA"-PROFESA LIPUMBA

Profesa Ibrahim Lipumba aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, amesema hana mpango wa kuhamia chama chochote pia hana mpango wa kuanzisha chama chake.
Profesa Lipumba amesema hayo katika kipindi cha Powerbreakfast kinachorushwa na Clouds FM alipokuwa akielezea msimamo wake juu ya CUF.
Katika mahojiano hayo Profesa Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alikosea kumnyima mkono Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuwa unapokwenda kwenye msiba jambo la msiba lilipaswa kutawala.
“Hata mimi nilipokutana na Maalim baada ya kunikatalia kurudi kwenye uenyekiti tulisalimiana.”

UBAKAJI HUU UNATISHA

Wednesday, 7 September 2016

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA HOTEL YA NYOTA 5 YA RAMADA ENCORE JIJINI DAR

Makamu wa Rais Mhe.Mama Samia Suluhu, leo amezindua hoteli nzuri na maarufu ya Nyota 5 iitwayo Ramada Encore Jijini Dar. Katika uzinduzi huo alikuwepo pia Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli hiyo Mhe.Abdul Ismail.

HII NDIO "MBEGE"; ASILI YAKE KILIMANJARO

Mbege ni kinywaji asilia cha wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro. Ni kinywaji chenye kilevi na hivyo chatumiwa tu na watu wanaozidi umri wa miaka 18. Katika kunywa kinywaji hiki, wakazi hawa kiasilia hutumia kifaa kiitwacho "kata" ambacho kinatokana na kibuyu kama unavyoona kwenye picha hapa chini. Kinywaji hiki hutengenezwa kwa ndizi mbivu zinazopikwa kwa muda mrefu kisha kuachwa kupoa kidogo, kisha kuwekwa kwenye kifaa maalumu kiitwacho "kihondi" au siku hizi hutumia pipa kubwa. Baadae huwekwa ulezi uliosagwa na kuachwa kwa siku kadhaa, kisha ukamuliwa-huchugwa kwa vifaa maalumu na kuwekwa ulezi uliopikwa kidogo na kuandaliwa tena kitaalamu. kisha huwa tayari kwa kutumika.