Tuesday, 12 July 2016

ASEMAVYO MHE HUMPHREY POLE POLE MKUU WA WILAYA YA UBUNGO BAADA YA KUAPISHWA

Hodi Ubungo, Hodi Ubungo, Hodi Ubungo
Mhe. Rais amenituma kuja kuwa Mtumishi na Kiongozi kwenu. Tuna kila sababu ya kuifanya Ubungo Wilaya ya Tofauti katika kila eneo na sekta, inawezekana. Hakika Ubungo Itakuwa Tofauti. Tushirikiane na Mungu atatubariki! Amina!
Wengine Mtashangaa, Nchi yetu, Taifa letu, Serikali yetu, Utumishi na Uongozi ambao tumepewa dhamana ni zaidi sana ya Matakwa binafsi. Serikali Ni Utamaduni, Ni Desturi, Ni Kanuni, Ni zaidi sana ya Matakwa yangu binafsi
Hodi Ubungo

NUKUU YA MANENO YAMHE RAIS MAGUFULI ALIPOKUWA AKIWAAPISHA WAKURUGENZI WA MIKOA NA WILAYA

"Ukiona unashangiliwa na adui, rudi nyuma kaangalie umekosea wapi, ukiona unapigwa vita na kukosolewa na adui, ujue umewapiga bao..."! JPJM 12 Julai 2016

MJUE NYEGERE: MNYAMA MWENYE WIVU KUPINDUKIA

Nyegere (Mellivora Capensis) ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea

Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa “limefaidi utamu” wa jike

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.

Nyegere ndio mmoja kati ya “fearless animal” duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama “defensive mechanism” yake.

Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na “upendo” wa Nyegere.

Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.

Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng’ata nyoka wa aina yoyote haponi.

Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere.

Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya

Monday, 11 July 2016

GARI ALILOTENGENEZA KIJANA MBUNIFU WA KITANZANIA JIJINI DAR

Gari aina ya Kaparata lililobuniwa na kijana mtanzania kutoka Gongo la Mboto Dar es Slaam Jacob Louis Kaparata (38).

Akizungumza wakati wa maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kaparata ameeleza kuwa alitumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchi kuunda gari hilo na kuwa miongoni mwa vitu hivyo vingine alivitengeneza mwenyewe na vingine alichukua vya aina nyingine ya magari.

Chassis nimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi nimelisuka kwa kutumia brake pipes zinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayo yanatumika kutengenezea mageti,” alisema Kaparata.

Injini, diff, gear box na matairi, vyote ni vya gari aina ya Suzuki Carry. Na nimelitengeneza kwa muda wa miezi mitatu na limenigharimu kiasi cha TZS 12,850,000.

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA KUPATA MRITHI BAADA YA KUJIUZULU JTANO HII

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kuwa Theresa May atakuwa waziri mkuu wa nchini hiyo baada ya yeye kuachia madaraka jumatano jioni

Theresa May ambaye alikuwa akipigia chapuo nchi hiyo kutojiondoa ndani ya Muungano wa Ulaya atairithi mikoba ya Cameron baada ya yeye kutangaza kuwa ataachia wadhifa huo kufuatia nchi hiyo kupiga kura ya kujitoa katika Muungano wa Ulaya.

May amebakia yeye kutwaa nafasi hiyo baada ya mwanasiasa Andrea Leadsom kujiweka pembeni kwa madai kuwa Uingereza inataka kiongozi imara na anaamini kuwa May anaweza kazi hiyo.
Waziri Cameron atahudhuria mkutano wa mwisho wa baraza siku ya Jumanne na atajibu maswali siku ya Jumatano asubuhi na jioni atakabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia.

MASANJA MKANDAMIZAJI KUUKACHA UKAPERA HIVI KARIBUNI

Miongoni mwa vitu vinavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na picha zinazomuonyesha Masanja Mkandamizaji akimvisha pete msichana anaedaiwa kuwa mchumba wake,kwenye picha hizo Masanja na mchumba wake huyo wanaonekana wakiwa kanisani na baadhi ya waumini akiwemo Mc Pilipili na Emanuel Mbasha.

PORTUGAL (URENO) MABINGWA WA UEFA EURO 2016

Hata baada ya kuumia goti la kushoto kwa Nahodha wao na mchezaji maarufu Cristian Ronaldo, Timu ya Taifa ya Ureno ilipata goli la ushindi muda wa nyongeza kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Eder
Eder akishangilia baada ya kuifungia Portugal bao la ushindi

Sunday, 10 July 2016

SHABIKI WA MWENDOKASI WA HAPA KAZI TU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni katika ziara zake alikutana na kijana aliyemshangilia kwa nguvu zake zote hali ambayo ilimfanya mkuu huyo wa nchi kumwita na kupiga naye picha.
Kijana huyo ambaye anaitwa Omar Abdalah Ramadhani ‘Mkereketwa wa Mwendokasi’ alisikika akisema “Magufuli kule aliko, aminia mzazi, Mungu akupe baraka zote mzazi, na asiyekupenda Mungu atamtokomeza, Watanzania tuko nyuma yako” kauli iliyomfanya Rais Magufuli amwite ili apige naye picha na baadaye kuombewa dua na kijana huyo.

Saturday, 9 July 2016