Sunday, 20 December 2015

MRADI WA UDART KUANZA KUTOA HUDUMA MUDA WOWOTE

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua eneo la karakana ya mabasi yaendayo haraka UDART iliyopo enero la Jangwani jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo Desemba 19, 2015.

Saturday, 19 December 2015

ROCK CITY SHOPPING MALL KUFUNGULIWA

Katikati ya Jiji la Mwanza kiko hiki kitu kizuri

Friday, 18 December 2015

HAPA KAZI TU YASHIKA KASI KWA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI WA MHE.JPM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amemtimua kazi mkandarasi anayejenga mfereji wa Buguruni kwa Mnyamani, Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kuujenga kwa kiwango kinachotakiwa. Mbali ya kuchukua hatua hiyo jana, pia Waziri Mhagama aliagiza mkandarasi huyo asilipwe chochote. Akiwa Tegeta, waziri huyo alimbana...

MHE RAIS MAGUFULI AFANYA KIKAO CHA MAWAZIRI WAPYA

Thursday, 17 December 2015

KOCHA JOSE MOURINHO WA CHELSEA ATUPWA NJE

Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya. The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita

VIDEO: MHE RAIS MAGUFULI ASEMA FEDHA KWA AJILI YA ELIMU BURE ZIMESHAPATIKANA


Ila picha hii ya mwanafunzi darasani inanifikirisha sana. Je wewe?

Wednesday, 16 December 2015

MHE.RAIS MAGUFULI APANGUA SAFU YA TAKUKURU

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Edward Hoseah

WAZIRI MKUU MHE.MAJALIWA AFANYA KIKAO NA MAWAZIRI/MANAIBU MAWAZIRI WAPYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri katika kikao cha kwanza cha kazi cha Baraza la Mawaziri alichokiitisha Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 15, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, 14 December 2015

RAIS DKT. MAGUFULI AMERUDISHA ENZI ZA HAYATI KARUME NA NYERERE – MZEE KUNDIHERI

WAZIRI MHE JENISTA MHAGAMA APOKELEWA WIZARANI KWAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 14, 2015 baada ya kuwasili ofisini kuanza kazi . Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (katikati), Naibu Mawaziri Dkt. Abdallah Possi (kulia) na Anthony Mavunde (wapili kulia)) baada ya mawaziri hao kuripoti Ofisini kwake kuanza kazi Desemba 14, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka, Wanne kushoto ni katibu Mkuu Kazi na Ajira, Eric Shitindi na watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikula.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu Mawaziri, Dkt. Abdallah Possi (Wapili kulia) na Anthony Mavunde (kulia) baada ya Waziri huyo na Manaibu wake kuripoti Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)