Thursday, 12 November 2015

VIDEO...MAKALA MAALUM: SIKU TANO ZA URAIS WA DK.JOHN MAGUFULI

MBIO ZA USPIKA WA BUNGE ZAANZA

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akizungumza na Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
WAKATI HUO HUO.................
Chanzo cha uhakika ndani ya CCM kimeieleza kuwa, walioonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ni aliyekuwa Spika wa Bunge la 10 Ni Anne Makinda, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge la 10, Mussa Azzan Zungu na Mjumbe wa Kamati kuu Dk. Emmanuel Nchimbi.

Wednesday, 11 November 2015

SERIKALI YA MAGUFULI KUPUNGUZA WIZARA, KUBANA MATUMIZI

Siku chache baada ya kufuta safari za vigogo nje ya nchi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli anakusudia kufyeka wizara 8 miongoni mwa 28 zilizopo sasa ili kubana matumizi.

Hatua hiyo ya Dr Magufuli ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwa wananchi wakati akijinadi kwenye kampeni zake za kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM kwamba atapunguza ukubwa wa serikali kwa kuunda baraza dogo la mawaziri.

Katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete, kumekuwa na malalamiko ya ukubwa wa baraza la Mawaziri huku baadhi ya wizara zikiwa na mawaziri watatu.

Kwa mkakati huo,endapo Dr Magufuli ataweza kufyeka Wizara 8, maana yake atakuwa amewatupa nje ya ajira vigogo zaidi ya 20 ambao ni mawaziri na manaibu wao pamoja na makatibu wakuu na manaibu wao ambao kasma zao za mishahara ni mzigo mkubwa kwa serikali

Baraza la kwanza la Rais mstaafu Kikwete mwaka 2005 lilikuwa na Mawaziri na Manaibu wao 60, jambo ambalo lililalamikiwa na wadau wengi kwamba halina tija bali lilikuwa na lengo la kulipana fadhila

Taarifa zaidi zinasema kuwa huenda Rais Magufuli akachelewa uteuzi wa mawaziri hadi Disemba mwaka huu ili kujipa muda zaidi wa kuangalia na kufanya uchambuzi wa wizara zipi za kuzifyeka kwani baadhi hazina tija

Tuesday, 10 November 2015

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU AKARIBISHWA RASMI OFISINI KWAKE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Nov 9, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Nov 9, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam

RAIS MAGUFULI AHUZUNISHWA NA HALI YA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

“ Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko” Amesema Balozi Sefue
mhe Rais Magufuli akimtazama kwa huruma Mama akiwa na mtoto wake wakiwa sakafuni katika Hospital ya Muhimbili

Sunday, 8 November 2015

VIDEO: ZIARA ZA VIONGOZI NJE ZAFUTWA KWA MUDA


Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi

Saturday, 7 November 2015

Friday, 6 November 2015

RAIS MSTAAFU DK.KIKWETE AONDOKA RASMI IKULU KUELEKEA MSOGA KUANZA MAISHA MENGINE

Rais Mstaafu Dk.Kikwete na Mkwewe wakiangana na wafanyakazi ofisi ya Rais Ikulu alipokuwa akiondoka rasmi katika Ikulu hiyo iliyopo Magogoni.
Akitoka kaatika Geti la Ikulu
Safari ya kuelekea Msoga nje kidogo ya Mji wa Chalinze kuanza maisha mengine baada ya kutumikia Taifa kama Rais kwa miaka 10

HAPA KAZI TU YAANZA RASMI: RAIS MAGUFULI AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ndg George Masaju ameapishwa rasmi asubuhi ya leo na Rais John P. Magufuli.
Uteuzi wa Mwanasheria huyo wa Serikali ulifanyika jana Novemba 5, 2015 mara tu baada ya rais Magufuli kuapishwa baada ya muda wa Serikali ya awamu ya nne kufikia kikomo.
(cHINI)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mkuu Othuman Chande,Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda

wAKATI HUO HUO..............................
mhe rais Magufuli amefanya ziara isiyo rasmi katika Wizara ya Fedha

Akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika Wizarani hapo

PICHA RASMI YA MHE.RAIS DK MAGUFULI

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiwaonesha waandishi wa Habari picha rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano