Ni juzi tu wamesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi yao, ila jana Zambia imempoteza Rais wao Mhe. Sata huko London alipokuwa akipata matibabu. Habari zinasema Makamu wa Rais Mhe. Dk, Guy Scottambaye ni wa asili ya Kizungu ndio anashika madaraka mpaka uchaguzi utakapofanyika tena. RIP Rais wa Zambia.
Watoto wana namna nyingi za kufanya matani ila matani mengine yahitaji ujasiri mkubwa kuyakubali . Hapa huyu mtoto akiamua kufanya majaribio ya matumizi ya hilo panga, anafungua bucha. Tuwafundishe watoto wetu matani mazuri na yafaayo katika kujijenga binafsi na jamii. Ila pia tuwakumbushe matani mengine ambayo yanaweza kuleta madhara.
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!