Saturday, 2 August 2014

EBOLA NA UKIMWI

Wakati ulimwengu bado unahangaika kutafuta tiba ya ugonjwa wa Ukimwi,sasa nayo Ebola yaibuka upya. Tunachojiuliza ni kuwa hivi kweli ni mtu alikaa kabisa akatengeneza hivi virus vya Ebola na Ukimwi kama sisi tunavyotengeneza vitumbua au maandazi kwaajili ya chai? Maana janga la Bomu la Atomic kule Nagasaki na Hiroshima Japani mpaka leo watu wanaathirika.Na bomu hili lilitengenezwa na binadamu kama sisi kwa hisia zake mwenyewe kuangamiza.

SAKATA LA KATIBA MPYA

Wednesday, 30 July 2014

HONGERA RAIS WETU MHE. J KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo ya kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa

HONGERA DIAMOND PLATNUMZ

Diamond Platnumz akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.

Tuesday, 29 July 2014

EID MUBARAK WADAU

Umati wa waamini wa kiislam waliohudhuria swala ya Eid el Fitr huko uwanja wa Maisara Zanzibar
Viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria swala hiyo
Swala ya Idd el fitr katika Masgid Maamur Upanga Dar
Swala na mawaidha katika uwanja wa Mnazi Mmoja Dar

Monday, 28 July 2014

VIMEPOTELEA WAPI VITABU HIVI?????

ENZI ZA MWALIMU......

Enzi za Mwalimu Nyerere hizi zilikuwa pesa halali na zenye thamani kubwa. Leo zimebaki kuwa urembo tu. Ipi tathmini ya thamani ya fedha yetu?

KWA RAHA ZAKO KAKA

VIONGOZI VIJANA MHE. JOSHUA NASSARI NA STEPHEN MASELE KUKUTANA NA MHE.RAISI OBAMA LEO

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni baada ya mahafali ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa kwa viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika yaliyokuwa yakifanyika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani
Ukumbi ambapo Mhe raisi Obama atazungumza na Vijana viongozi wa Afrika wanaoonyesha dira (the most promising young African leaders)