Friday, 7 March 2014

MALEZI YATAKA MOYO

Unapoingia katika maisha ya majukumu ya kifamilia, Mambo kama haya ya mtoto kwa mzazi hayakwepeki. Jipange sawasawa.

MWANAMKE MWENYE UMRI MKUBWA KWA SASA DUNIANI

Misao Okawa, ambaye aliwekwa kwenye kitabu cha rekodi kubwa za dunia ‘Guinness’ mwaka jana kama mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani, juzi (March 5) amefanya sherehe ya siku ya kuzaliwa baada ya kufikisha umri wa mika 116.
Misao ambaye anaishi chini ya uangalizi na matunzo huko Osaka, Japan alitangazwa rasmi kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kufariki.
Ingawa umri wake ni mkubwa sana, anaonekana bado ana afya nzuri na aliweza kuipuliza mishumaa yake kama mtu mwingine.

Hata hivyo yawezekana kuna watu wenye umri mkubwa zaidi yake sehemu fulani duniani ila kwakuwa hawajaweza kufikiwa na vyombo vya habari imekuwa ngumu kuwatambua. Mungu ana yake mengi hatuwezi jua yote.

Thursday, 6 March 2014

KULIKONI BUNGE LA KATIBA?!!!


Wabunge wa bunge la Katiba wakitoka ktk ukumbi wa Bunge Dodoma leo baada ya hali ya kutofautiana miongoni mwa wabunge. Hii Katiba mpya tutaipata kweli kwa mtindo huu?

Wednesday, 5 March 2014

NANI KAMA MAMA?

Tunapomtazama na kumzungumzia mwanamke alopewa heshima ya kuitwa mama wa dunia au mlenzi wa Ulimwengu twamtazamaje? Je twamwona kama mtu duni asiyeweza chochote? dhaifu asiyeweza Fanya maamuzi magumu? mwenye wivu na msaliti ?
Mwanamke yeyote anastahili sifa na heshima za kipekee. Wakati mwingine hatujui ni kwa namna gani kinamama wamejitolea kuhakikisha maisha yanakuwa mema kwa wale wanaowahusu. Ila na kwa dada zetu wanaochipukia wasipoteze thamani ya mama duniani kwa matendo yasiyostahili kwenye jamii hata kushusha hadhi.

Saturday, 1 March 2014

MWONEKANO WA MADINI YA TANZANITE


Haya ni madini yanayopatikana nchini Tanzania pekee eneo la Mererani,Simanjiro Arusha.Hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani tofauti na Tanzania. Tujivunie fahari ya Tanzania.

VITUKO: MTU AKIFANYIWA MASSAGE NA TEMBO.


Hii yataka moyo kwakweli

Friday, 28 February 2014