Saturday, 11 January 2014

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.

Tunakumbushwa kutimiza wajibu wetu kama wazazi au walezi kwa watoto. Wakati tukijionea matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu,umaskini na uvunjifu wa amani katika jamii,ni dhahiri msemo huo hapo juu wajidhihirisha. Mtoto akilelewa vizuri,hukua vizuri katika nyanja zote za maisha. Lakini asipolelewa vizuri ni chanzo cha vurugu katika jamii. Mtoto huyu anachomeka misumari hii kwenye Yeboyebo ambapo baadae ni hatari kwa wenzake na hata yeye mwenyewe Watoto hawa waonekana kuridhika na walilofanya lakini huku ni.kukosa malezi na tabia hii ikiachwa huzalisha wakorofi, wavutaji bangi,vibaka,majambazi na watu wengine hatari kwa jamii. Kwa upande wa wasichana wasipopata malezi mazuri waweza kufanya hayo nilotaja na hata kujiingiza katika matumizi mabaya ya miili yao kama "machangudoa" tangu wadogo (picha hii ya binti aliyekamatwa akijiuza huko Mwanza ni kwa hisani ya Global Publishers).

DUNIANI KUNA MAMBO: 1. HUYU NDIE NABII HUKO BRAZIL ANAYEJIITA "YESU" 2. WAAMINI WAAMRIWA KULA MAJANI/NYASI

Inri Cristo, 66,  akiongea na wanafunzi (wafuasi) wake nje ya kanisa lake liliopo Brasilia nchini Brazil. INRI ni neno la kilatini lenye maana "Yesu Mnazareti,Mfalme wa Wayahudi" kama kibao kilichoweka juu ya msalaba wa Yesu kilivyosomeka nyakati zile. Na mchungaji mmoja huko Afrika Kusini katoa mpya akiwaamuru waumini wake kula majani/nyasi kama namna ya kumkaribisha Mungu maishani mwao. Mchungaji  Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries katika mji wa  Pretoria nchini Afrika ya Kusini kawambia waumini watoke nje wale majani ili wawe karibu na Mungu. Ila sijui kama waumini hawa wameyasoma vizuri maneno ya Yesu mwenyewe kwenye biblia Mathayo 24:11 "Watatokea manabii wengi......"

Thursday, 9 January 2014

SERIKALI ITAZAME HILI:KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Basi la kampuni ya Mtei Express T 742 ACU linalofanya safari zake kati ya Singida na Arusha leo limeteketea kwa moto baada ya wananchi wachache wa kijiji kimoja huko Singida kulichoma moto. Hii inafuatia ajali ya pikipiki Aina ya SkyGo T 368 BXZ ambapo basi hilo liligongana na pikipiki ilokuwa na abiria wanne na watatu kati yao ambao ni wa familia moja kufariki dunia. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea leo saa moja na dakika moja asubuhi huko katika kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Mkoani Singida Ila ni budi wananchi kuacha tabia ya kujichukulia maamuzi bila kushirikisha vyombo vya dola. Pia Blog hii inawaasa wananchi wote kuwa makini hasa watumiapo vyombo vya moto au kuwepo barabarani.

Tuesday, 7 January 2014

SHUKURU ULIVYOUMBWA

Huyu ni mwanadada ambaye sehemu kubwa ya maumbile yake yanaonekana ya kiume. Mwanaume huyu kutoka Indonesia anasumbuliwa na vipele hivi tangu miaka ya 90 baada ya kufanyiwa upasuaji fulani kiunoni.

Monday, 6 January 2014

JEURI YA FEDHA

Jumba la kifahari la mwanamuziki Rihanna huko Los Angeles. Gari la kifahari aina ya Range Rover iliyopambwa nakshi na sarafu za dhahabu huko Uarabuni Kampuni ya magari ya Marcedes Benz yatoa gari inayojiendesha yenyewe. Meli kubwa na ya kifahari yenye huduma za kila namna ndani

PILIKA ZIMEANZA

Juma jipya la kwanza la mwaka huu lililo kamili limeanza. Kila mmoja yupo ktk kutafuta kipato kwa njia halali. Nawatakia wadau wote na watafutaji halali kila jema ktk kuboresha maisha kwa mwaka huu. Ila kwa wale waliopewa dhamana mbalimbali katika jamii,ni muhimu katika kuwajibika kwao waangalie adha hii wanayopata baadhi ya wananchi ktk maisha yao ya kila siku. "something should be done because this is not fair"