Saturday, 16 May 2009

HUYU NDIYE HAYATI IDD AMIN DADA

Inasemekana kuwa Serikali ya Uganda ina mpango wa kutulipa fidia Watanzania kwa kumwangusha Dikteta Idd Amin kutoka madarakani mwaka 1979 katika vita ile ya Uganda. Hayo yamesemwa na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Mhe.Eriya Kategaya,akisema hii itakuwa kama ishara tu ya shukrani kwa namna ambavyo Watanzania chini ya Hayati Mw. J.K. Nyerere walivyojitolea fedha, mali na maisha yao kuhakikisha Nduli Idd Amin anaondoka madarakani na nchi yaa Uganda inakuwa na amani.

SHERIA MKONONI KATIKA KUTOA HUKUMU

Ukisikia mtu anasema utajuta kuzaliwa, basi ndo katika masuala kama haya. Hapa kijana huyu ameponea chupuchupu kugeuka "ndafu" baada ya wananchi wenye hasira kutaka kumchoma moto. Tuache mtindo wa kujichukulia sheria mkononi japo wakati mwingine inasababishwa na hasira. Huyu nae ni binadamu japo katika mapungufu yake.


Thursday, 14 May 2009

BORA NYUMBANI!!

Mambo kwa wenzetu ndo kama hivyo tena tehe tehe tehe tehe



Wednesday, 13 May 2009

TUITE TUKUPAMBIE SHEREHE YAKO

Hawa ni magwiji wa upambaji Tanzania. Waweza kuwasiliana nao kupitia www.decorplacetz.blogspot.com. Wapo United Nations Road (opp. Tambaza High School, Nextdoor to Flying Chefs. Cell: +255 713 243 174/0784 553 679








NYUMBANI KWA RAIS WETU

Hii ndiyo nyumba ambapo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa na kukulia. Ni katika nyumba hii iliyopo katika kijiji cha Msoga,Bagamoyo kilomita 10 toka Chalinze-Tanzania .

BARABARA ZETU: BADO KAZI IPO

Wakati tunaipongeza Serikali yetu kwa juhudi kubwa katika ujenzi wa barabara nchini, pia tunazidi kuiomba serikali itupie jicho sehemu hizi nyingine pia ambazo zina barabara korofi hasa nyakati za mvua. Shughuli nyingi za maendeleo zinakwamisha na ukosefu wa barabara za kufikika kirahisi kama inavyoonyesha katika picha magari yakiwa yamekwama katika Barabara ya Lindi/Mtwara hivi karibuni.

Barabara ielekeayo Mbagala = tambarare

Barabara Lindi/Mtwara = korofi

MAENDELEO YA SIMU ZA MKONONI

Tulianzia hapa kwenye Motorola 8500X tukiwa na simcard/line ya Mobitel au Tritel

Kwa sasa tupo hapa kwenye Motorola Razr na simcard/line zetu za Vodacom, Zantel, Tigo na Zain

Au pengine hapa kwenye Samsung

Au pengine kwenye hii NOKIA

Tuesday, 12 May 2009

HONGERA KIJANA WA NYUMBANI

Uzalendo umenishinda, imenibidi nimsifie hadharani Kijana mwenzangu wa nyumbani kwa kufaulu vyema. Hongera sana na Asante kwa kutuwakilisha vyema wanaSIHA na KYENGIA-KILIMANJARO

"double click" picha kukuza maandishi

Monday, 11 May 2009

BABA MTAKATIFU NCHINI JORDAN

Baba Mtakatifu Benedicto XVI jana ameingia Jordan kwa ziara ya kwanza Mashariki ya Kati.

Papa akisalimiana na Mfalme Abdullah wa Jordan