Bango lililopo juu ya Mlima Kilimanjaro Mlima kilimanjaro unavyoonekana ukiwa Horombo Hut Mlima Kilimanjaro unavyoonekana ukiwa katika uwanda wa chini Mwanga na Same Mlima Kilimanjaro unavyoonekana ukiwa Sanya Juu-Hai
Watoto wa nyumbani ni wabunifu sana. Hawataki kuachwa nyuma katika michezo mbalimbali. Hapa wanacheza "Pool table" ambao huko ughaibuni unaitwa "Snooker"
Baba wa nyumbani Rais J.Kikwete karejea nyumbani leo akitokea ziarani Saudia. Hapa ni Mheshimiwa Makamu wa Rais Dk.Shein akimpokea uwanja wa ndege. Kwa nyuma ni Mama Salma Kikwete
Picha hizi mbili zaonyesha namna tofauti za ubebaji wa watoto. Najaribu kujiuliza ni njia sahihi, na kama ndio pia ni ipi inaonyesha zaidi upendo wa mama kwa mtoto? Wanablog nisaidieni jibu.
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!