Sunday, 11 December 2016
MELI YENYE MALORI 600 YA DANGOTE YAWASILI MTWARA
Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote jana alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini; Alitamka kuleta malori 600 kwa ajili ya usambazaji wa DANGOTE CEMENT na hii ni fursa ya ajira kwa madreva 600
Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema leo meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini. Ameongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 imetia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.
Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako