Leo Kanisa Katoliki kupitia kiongozi wake Mkuu duniani Baba Mtakatifu Francis 1 amemtangaza Mama Teresa wa Calcuta raia wa Albania kuwa MTAKATIFU. Raia huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997 alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.
Atajulikana kuwa mtakatifu Teresa wa Calcutta.
Waandishi wnasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis kuhusu kanisa linalojikakamua kuwasaidai watu masikini.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa ,na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu masikini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.
HISTORIA
Jina halisi la Mama Teresa lilikuwa Agnes Gonxha Bojaxhiu, mwenye asili ya Albania aliyezaliwa 1910 katika eneo ambapo sasa linatambuliwa kama Skopje, Macedonia.
Alifika India mnamo 1929 baada ya kuishi na kundi la wamishenari kwa muda nchini Ireland.
Alianzisha kundi la Wamishenari wa Misaada mnamo 1950 na akapewa uraia wa India mwaka uliofuata.
Mnamo 2015, alisifiwa na wataalamu wa Vatican kwa kusababisha uponyaji wa mwanamume wa Brazil katika mwaka wa 2008 ambaye alikuwa na uvimbe kwenye ubongo wake.
Hiyo ilimfanya Teresa kufikisha kiwango kinachohitajika kwa mtu kutangazwa kuwa mtakatifu.
Papa John Paul wa Pili alimtangaza kuwa mbarikiwa mnamo 2003.
Francis aliwahi kukutana na Teresa 1994.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako