Mahakama ya Mkoa wa Manyara imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali, ikiwamo ngozi ya chui na nyoka aina ya chatu.
Washtakiwa hao ni Mathayo Mchono, Bura Massay, wakazi wa Gembaku wilayani Mbulu na Bryson Jacob wa Bashey wilayani Karatu.
Hakimu Bernad Nganga amesema leo kuwa mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuwatia hatiani washtakiwa hao.
Hakimu Nganga amesema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani.
Awali, waendesha mashtaka, Linus Bugaba na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari waliiomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako