Thursday, 31 March 2016

WABUNGE 3 KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU yawaburuza Mahakama ya Kisutu wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge wanaotuhumiwa kwa Rushwa. Mh.Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa,Mh.Sadiq Murad Mbunge wa Mvomero na Mh.Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara

UJUMBE KWA KINADADA WAFANYAO KAZI MAOFISINI

Akina dada nipende kuwashauri kitu kimoja.

Msipende kuwadharau vijana mnaofanyanao kazi ofisi moja na kuwaona wa thamani kubwa watu msiowajua hasa wa kwenye mitandao mkidhani kuwa hao ndio wana maisha bora.

Ukweli ni kwamba akina dada wengi wanatabia ya kuwadharau vijana wanaoishinao wakiamini kwamba watawapata watu wenye sifa wanazozihitaji toka kwenye mitandao ya kijamii.

Matokeo yake kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wasiokuwa na baba au kwa jina maarufu kama watoto wa love connect, wakishazalishwa huko walikokimbilia na kuachwa ndio wanawaona wa thamani kubwa hawa waliowaacha mtaani.

Ushauri kwa wadada acheni tamaa rizikeni na vijana mnao ishi nao kwenye mazingira yenu kwani wengi wao ni watu wenye nia nzuri kwenu.

JAPAN YAIPA TANZANIA MSAADA WA BILIONI116.4

Wakati siku chache tu zimepita tangu Marekani kupitia MMC kuiondolea Tanzania Msaada ilokuwa imepangiwa, basi mwenye bahati huyu kapewa msaada mwingine na Japan
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili unahusu masuala ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500

Tuesday, 29 March 2016

TANZANIA NA KUWAIT WAKUBALIANA KUWA NA SAFARI ZA ANGA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan.

MHE RAIS MAGUFULI ATEMBELEA CHATO ALIKOZALIWA MARA YA KWANZA TANGU AWE RAIS

Akiwa njiani kuelekea Chato Geita, Mhe.Rais Magufuli na msafara wake walifanya "suprise" kwa kuingia mgahawani na kupata lunch.
Baada ya kufika mjini Chato, mhe.Rais Magufuli aliwahutubia wakazi waliofika kumsikiliza

Monday, 28 March 2016

NAWATAKIA PASAKA NJEMA

Mhe rais magufuli akisalimiana na Askofu Dk Alex Malasusa(KKKT) Mkuu wa Dayosisi ya mashariki na Pwani alipowasili katika Kanisa la Azania Front kuhudhuria Ibada ya Pasaka leo

Saturday, 26 March 2016

JOTO LA DAR ES SALAAM KIBOKO YAO

Mpaka wakati mwingine inafika mahali najiuliza hivi jiji la Dar lipo katika hii hii sayari ya dunia au?

Friday, 25 March 2016

WAKRISTO DUNIANI POTE WAFANYA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA YESU MSALABANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuubusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016

MHE. RC. MAKONDA APATA BARAKA ZA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI NCHINI

Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao ambapo jana alimtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa ajili ya kupata baraka na busara zake
Apostle Onesmo Ndegi,Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Mh. Makonda .

Wednesday, 23 March 2016

KWA MWANAUME ANAYEJITAMBUA VIZURI: HILI SIO SAHIHI

Ukitazama picha hii kwa makini utaona namna ambavyo mwanamama huyu akiteseka na mizigo na mtoto mgongoni huku mwanaume pembeni anatembea bila mzigo wowote. Kama huyu ni Baba wa familia, basi hiyo nyumba ina unyanyasaji mkubwa wa kijinsia.Yaani hata mnyama kabeba mzigo ila mwanaume kama mfalme vile. Yamepitwa na wakati hayo.

BARUA ZA WAZI ZA WAH:ZITTO na BASHE KWA MHE SPIKA KUJIUZULU KUWA MJUMBE WA KAMATI

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishutumu Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe wamepokea rushwa.
Alichokiandika Zitto: “Kutokana na shutuma hizo ameamua kumuandikia spika barua ya kujiuzulu na kumtaka achunguze na kuchukua hatua.”
Hii ni nakala ya barua yake aliyomwandikia Mhe.Spika wa Bunge

Tuesday, 22 March 2016

MEYA MPYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ASHINDA KUTOKA UKAWA(CHADEMA)

Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam umekamilika leo katika ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Mwita ameibuka na ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata kura 84 akimshinda mpinzani wake, Yenga Omary wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 67.

Uchaguzi huo umeweka historia ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi (1992), Chama Cha Upinzani kimepata nafasi ya kuongoza jiji hilo.

Uchaguzi huo uliahirishwa mara kadhaa kutokana na mvutano uliokuwa unaibuka kati ya wajumbe wa CCM na Chadema na kuzua vurugu wakati mwingine.

Tofauti na ilivyo kwa tarehe nyingine za uchaguzi zilizopangwa na kuahirishwa wakati wajumbe wakiwa ukumbini, viongozi wa ngazi za juu wa Chadema pamoja na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa walihudhuria kushuhudia uchaguzi huo.

LEO KUMETOKEA TERRORIST ATTACK NCHINI BELGIUM

Asubuhi ya leo kumetokea mlipuko wa Bomu la kujitoa mhanga huko Ubelgiji katka Uwanja wa Ndege cha Zaventem, Brussels na Kituo cha treni za Metro na inasemekana watu 30 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 180 kujeruhiwa. Kikundi kimoja cha kigaidi kimejitangaza kuhusika na milipuko hiyo.

MABASI YAENDAYO KASI KUANZA KUFANYIWA MAJARIBIO WIKI HII ILI YAANZE KUTUMIKA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze kuzoea njia na taa za kuongozea magari.

“Wataanza na mabasi kati ya 30 – 50 ambayo yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao, hivyo waanze kuzoea,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi

MHE DK MOHAMED SHEIN ATANGAZWA MSHINDI KURA ZA URAIS ZANZIBAR

March 20 2016 ilikuwa ni siku ya ambayo Wananchi wa Zanzibar walipata fursa ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wao, na hii ni baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa awali uliofanyika october 25 2016.
Leo March 21 Tume ya Uchaguzui Zanzzibar imetangaza matokeo ya uchaguzi huo ambapo imemtangaza mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein kuwa Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa asilimia 91.4%
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipokea cheti maalum cha Ushindi wa Uchaguzi wa marudio kutoka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

Sunday, 20 March 2016

HONGERA MHE CHRISTOPHER OLE SENDEKA

Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji mpya wa CCM kuanzia leo.Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar.Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Ndugu Nape Nnauye ambapo kwa sasa Olesendeka pichani kati ndiye ameishika nafasi hiyo.

UCHAGUZI MKUU WA MARUDIO ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo namba 1 cha kupiga kura namba 1 Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo

Saturday, 19 March 2016

NAPITA TU: MUONEKANO WA HARUSI MIKOANI

Bw na Bi Harusi huko Musoma
Bw na Bi Harusi huko Kilimanjaro
Bw na Bi Harusi huko Singida
Harusi Mikoa ya Pwani mwa Bahari ya Hindi
Bw na Bi Harusi huko Kagera

"NAONA AIBU KUISHI KWENYE JIJI LENYE HALI HII".... RC MAKONDA


RC Mpya wa Mkoa wa Dar es Sallam Mhe.Paul Makonda leo amekutana na Wenyeviti wa Mitaa na Maafisa Watendaji wa Mkoa huo kujadiliana nao mambo mbalimbali huku akisema anaona aibu kuishi kwenye Jiji lenye kero zote hizi ilihali Wenyeviti wa Mitaa wapo.

NSSF,TBC, NA RAHCO WAPATA WAKURUGENZI WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).

Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.