Leo Februari 20 ndio siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka la Tanzania, kwani ndio siku ambayo mashabiki wa soka la Tanzania wamepata nafasi ya kushuhudia mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, baada ya mchezo wa mzunguuko wa kwanza kumalizika kwa Yanga kuifunga Simba goli 2-0.
Dk 90+ 3: Mpira umemalizika, Yanga SC inaifunga Simba SC 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Donald Ngoma kipindi cha kwanza na Amissi Tambwe kipindi cha pili
Dk 90+ 1: Yanga wanapata kona ya kwanza, lakini haina faida
Dk 87: Simba SC wanapata kona tena inazua kizaazaa langoni mwa Yanga kabla ya kuondoshwa kwenye hatari
Dk 82: Mashabiki wa Simba SC wanaanza kuachia siti zao Uwanja wa Taifa
Dk 80: Brian Majwega anakwedna kuchukua nafasi ya Ibrahim Hajib
Dk 72: Tambwe anaifungia Yanga bao la pili kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Godfrey Mwashiuya kutoka kushoto
Dk 45: Hassan Kessy anapiga mpira wa adhabu unapotea
Dk 44: Simba wanapata kona ya saba wanapoteza pia
Dk 44: Simba wanapata kona ya sita wanapoteza
Dk 39: Ngoma anaifungia Yanga bao la kwanza. Hassan Kessy alimrudishia pasi fupi kipa Vincent Angban, Ngoma akainasa akampga chenga kipa huyo na kufunga
Dk 35: Simba SC wanapata kona nyingine dakika ya 35, lakini inaokolewa
Dk 25: Abdi Banda anaonyeshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu tena Ngoma
No comments:
Post a Comment
Maoni yako