Monday, 11 January 2016
VIDEO:MHE.MAALIM SEIF ATOA MSIMAMO KUHUSU UCHAGUZI ZANZIBAR
MGOMBEA KITI CHA URAIS ZANZIBAR KUPITIA TIKETI YA CHAMA CHA WANANCHI CUF MAALIM SEIF muda mchache uliopita amezungumza na waandishi wa habari: Na zifuatazo ni sehemu ya nukuu za kauli alizotoa leo kwenye tamko lake:-
"Uchaguzi ulifanyika katika mazingira ya amani, utulivu bila kutokea vurugu, waangalizi wote walisifu. Kitendo cha kufuta matokeo kimeitumbukiza Zanzibar kwenye matatizo makubwa ndani na nje ya nchi"
"Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi alivunja katiba juu ya utaratibu wa Tume kufuta uchaguzi bila kushauriana na Tume (akatoa ufafanuzi juu ya muundo wa Tume)"
"Tume haikutangaza kurudiwa kuhesabiwa kura kwa kuwa hakukuwa na kasoro yoyote kwenye uchaguzi, si M'kiti wa Tume wala Tume yenyewe haina mamlaka ya kuhoji matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi"
Mgombea huyo Urais wa Chama cha CUF Zanzibar, Maalim Seif amehitimisha mazungumzo yake na waandishi wa habari kwa kusema kuwa hatokubali uchaguzi huo kurudiwa, akisisitiza kuwa uchaguzi kufutwa ni batili.
Asema ataendelea na mazungumzo ya kupata suluhu na hawezi kuwasaliti Wazanzibari.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako