Wakati huo huo inasemekana kuwa...Waziri Mkuu mstaafu, Monduli, Edward Lowassa ametajwa kuongoza katika kutaja vipaumbele vya maendeleo ikiwamo kupunguza tatizo la Ajira nchini na kuinua Elimu, miongoni mwa kundi la wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kadhalika, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa ndiye kiongozi wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba zake kuliko wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.
Hayo yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini
No comments:
Post a Comment
Maoni yako