Tigo Tanzania imetangaza mgao mwingine wa malipo kutoka kwenye mfuko wa fedha wa Tigo Pesa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 (US $ 1.8) kwa wateja wake. Mgao huu wa fedha ndio wa kwanza katika robo wa mwaka huu.
Malipo haya ni ongezeko la asilimia 6 ukilinganisha na mgao uliopita wa bilioni 3.1 uliotolewa katika robo ya mwaka iliyopita 2014. Ongezeko hili linaashiria ukuaji wa umaarufu wa huduma hii pamoja na ongezeko la idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa, kwa mujibu wa maelezo ya Kaimu Meneja Mkuu, Cecile Tiano.
“Tunayofuraha kubwa sana tena kutangaza ugawaji wa faida hii kwa watumiaji wetu wa Tigo Pesa. Malipo haya yanadhihirisha moyo wetu wa kushiriki katika kuboresha hali za maisha wateja wetu pamoja na nchi zima kwa ujumla,” alisema Tiano.
Alisema kwamba malipo haya ya robo mwaka yatalipwa kwa watumiaji wote wa huduma ya Tigo Pesa ikiwemo mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na mteja mmoja mmoja.
“Tunaamini ya kwamba faida hii ya robo ya kwanza ya mwaka 2015 itatoa nafuu ya kifedha kwa mamilioni ya wateja wa Tigo kutokana na mahitaji na matumizi yao waliyonayo,” alisema.
Meneja Mkuu alielezea, kama ilivyokuwa awali ya kwamba wastani ya kiwango amabacho mteja atajipatia itatokana na kiwango ambacho atakuwa alikuwa anakihifadhi katika akaunti yake ya Tigo Pesa.
Tigo Pesa ilikuwa huduma ya kwanza ya kifedha ya simu ya mkononi duniani kulipa mgao wa faida kwa wateja wake pale mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulipozinduliwa kutoa migao yake ya fedha rasmi mwezi Julai 2014. Mgao unaofuata war obo mwaka wa fedha wa mwezi Aprili mpaka Juni 2015 utalipwa mwezi Julai mwaka huu, kutoka na maelezo ya Meneja Mkuu.
Mgao wa faida kutoka mfuko wa fedha wa Tigo Pesa inaenda sambamba na tangazo la Benki Kuu lilitolewa mwezi Februari 2014. Mpaka sasa kampuni imekwisha lipa kiasi cha shilingi bilioni 23.9 kwa watumiaji wa Tigo Pesa katika migao minne tofauti ya robo mwaka tangu kuzinduliwa kwa huduma hii Julai 2014.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako