Katika Ibada ya Jumapili ya Pasaka, Baba Mtakatifu Francis 1 ameiombea dunia Amani na hasa akieleza kuhuzunishwa kwake kwa kitendo cha wanafunzi zaidi ya 150 kuuawa kikatili katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya mwishoni mwa juma,mauaji yaliyolenga wanafunzi wakristo. Amesisitiza makubaliano ya amani katika pambe nyingi za dunia yafanyike kuendelea kuleta amani katika nchi zenye machafuko.
Kiongozi huyo anaongoza zaidi ya waumini Bilioni 1.2 duniani wa madhehebu ya Kikatoliki.
Akitoa ujumbe wake wa Pasaka mbele ya umati mkubwa katika medani ya Saint Peter's, Vatican, Papa Francis alitoa wito kwa mateso dhidi ya Wakristo dunia nzima kukomeshwa.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako