Pengine nimeonelea ni vizuri kujikumbusha mambo yalivyokuwa miaka kadhaa ilopita ili iwe changamoto kwa kizazi cha sasa. Ni vizuri kujua tulikotoka ili kama kuna mazuri tuige au mabaya tuzidi kuepa. Nawaletea picha hizi ila kwa lengo la kuburudisha tu zaidi.
Kibatari
kwa wengi walio mjini pengine kitakuwa ni kitu kipya kwao maana umeme ndo unatumika zaidi. Lakini siku za nyuma na kwa wengi walio vijijini ambako huduma za umeme hakuna, hiki ndo kifaa cha kuleta mwaka wakati wa usiku.
Siku hizi matumizi ya fedha hizi hakuna tena na hata matumizi ya sarafu yamepungua sana. Lakini hii ni moja ya sarafu zilizokuwa zinatumika kwa malipo halali ya senti 5.
Santana
Ilikuwa ni kawaida siku hizo zilizopita inapofika wikiend kama hii basi mwanaume anavaa viatu hivi na suruali inayoitwa pekosi huku amechana mywele zake kwa staili iliyojulikana kama Afro, anatoka kwenye kutembea viwanja, pengine ni pale Mwafrika Bar au sehemu walipo akina Sikinde Jazz Band.
Mvulana ulipofanikiwa kupata hela kidogo hasa kijijini ukanunua kaseti hii aina ya Panasonic basi Kijiji kizima kitajua, maana kanda za Pamela Nkuta na Yondo Sista zitapigwa siku nzima
(Tutaendelea toleo lijalo usikose)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako