USALAMA WA MAISHA YAKO.
* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua.
Hiyo ni hatari kwani hujui huyo
jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi
ya wizi au mauaji. Inawezekana
simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige
sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake
kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina
sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa,
unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha
unaichana. Unapoitupa, watu
wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya
vocha ile na kuweka sehemu ya
tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na
wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina
lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya
matukio hayo yakitokea na namba yako
kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa
namba moja. Wengi wamepewa kesi
za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini,
wanapoona vidhibiti wanakuchukua
kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni
makini ili usije kuingia matatizoni,
simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi
kama uzembe, utaishia pabaya.
MPE ONYO NA MWENZAKO.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako