Tukiangalia taswira hii tunapata mengi ya kujifunza. Miongoni mwa hayo ni:-
"Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" Mtoto huyu japo katika udogo wake kashaanza kuiga wanachokifanya wazazi au ndugu zake. Yaelekea atakuwa mama mzuri katika mapishi. Ila pia yawezekana akawa mchuuzi mzuri wa biashara ya samaki. Yaelekea pia atakuwa mwajibikaji mwenye kujituma hata katika mazingira magumu kama aonekanavyo hapo bila nguo juu na joto kali la moto.
Ila pengine ni vizuri pia tukaangalia madhara anayowezapata huyu mtoto. Kwanza yaonesha kuna dalili fulani za mzazi au mlezi kuzembea kidogo maana mtoto wa umri huu si vyema kuwa katika mazingira hayo,tena bila uangalizi. Na pili kiafya joto hilo linaweza kuidhuru ngozi ya mtoto huyo ambaye hajajisitiri vizuri. Tuwe waangalifu.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako